Ulemavu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 26:
Ulemavu wa kiakili unatokea kwa viwango tofauti sana. Mara nyingi hautambuliki hadi mtoto anaingia shule na kuchelewa kujifunza. Hata hapo ni lazima kutofautisha kama tatizo ni ulemavu wa akili au ulemavu wa kujifunza tu. Wengine wanaishia kiwango cha elmu kinacholingana na uwezo wa mtoto wa wastani mwenye miaka 9-12<ref>[http://www.aafp.org/afp/2000/0215/p1059.html Identification and Evaluation of Mental Retardation, American Family Physician, Feb 15, 2000]</ref> na wanaweza kujifunza kazi inayowawezesha kudumisha maisha yao wakiwa watu wazima.
 
==Haki za watu wenye ulemavu==
Mwaka 2006 Umoja wa Mataifa ulianzisha [[Mkataba wa kimataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu]] (UN Convention on the Rights of Persons with Disabilities UNCRPD) kwa shabaha ya kulinda na kuboresha hali ya walemavu milioni 650 dunani. Hadi mwaka 2015 mataifa 159 yalita sahihi mkataba huu na 154 kati yao yaliidhinisha hatua hii. Mataifa yanayokubali mkataba huu yamepokea wajibu wa kuhakikisha haki sawa za elimu, ajira, kumiliki mali na kuoa sawa na watu wote. Ni marufuku kuwatumia bila kibali kwa majaribio ya kiganga.
 
Taasisi na shirika mbalimbali zinafuatilia jinsi gani mashariti haya yanatekelezwa na serikali mbalimbali. Katika Afrika ya Mashariki kuna kwa mfano United Disabled Persons of Kenya (UDPK) au Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.
 
Nchini Tanzania katiba ya 1977 ilitambua haki za watu wenye ulemavu na kukataza aina zote za ubaguzi. Mnamo mwaka wa 2004, Wizara ya kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo ilitoa Sera ya Taifa ya watu wenye Ulemavu, inayosisitiza kujitolea kwa wizara hiyo katika kuhakikisha kwamba kuna haki sawa kwa watu wenye ulemavu.
 
==Marejeo==