Ubalehe : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 39:
[[Mapumbu]] yanaanza kutengeneza [[mbegu za kibinadamu]] kwa wingi sana: hizo ni ndogondogo na zina umbo kama la [[viluwiluwi]] vya [[chura]], yaani vina vichwa na mikia tu.
 
Vichwa ndivyo vinavyoleta [[viini vya urithi]] wa baba. Mikia kazi yake ni kusaidia tu kusukuma mbegu kwa kuogelea ndani ya [[tumbo la uzazi]] mpaka zikutane na [[kijiyai]] cha [[mama]], halafu inapotea ndani ya kijiyai. Mbegu zikiwa tayari zinahifadhiwa kwanza katika [[kifuko cha akiba]], karibu na kibofu, zikisubiri msisimko wa kijinsia ili zitoke kwa njia ya uume na kuanza mashindano ya kutafuta kijiyai, zikisaidiwa na majimaji ambayo yanaitwa [[shahawa]] na kutengenezwa ndani ya kifuko. Shahawa inafuata [[mshipa wa mkojo]] bila ya kuchanganyikana nao.
 
Shahawa inaweza ikatoka hata nje ya tumbo la uzazi la [[mke]], lililo [[shabaha]] yake, kwa kuwa inalenga [[uzazi]] hasa. Inaweza ikatokea k.mf. kutokana na [[ndoto]] za usiku, bila ya mtu kukusudia; huyo anaweza akazinduka mara au kutambua [[asubuhi]] tu kilichotokea. Kwa vyovyote asihangaike kwa kuwa hilo ni jambo la kawaida lililopangwa na [[Mungu]] ili kumsaidia [[mwanamume]] asiye na mwenzi. Maana mbegu zake kadiri zinavyoongezeka katika kifuko cha akiba zinataka kutoka, hivyo zinamuelekeza kwenye matendo ya kijinsia. Basi, kwa ndoto hizo mbegu zinapungua bila ya dhambi, na [[vishawishi]] vinakosa ukali wake. Ni suala la kusubiri tu na kuwa na hakika kwamba havitadumu muda mrefu kwa nguvu ileile.
Mstari 47:
Mvulana anapotokwa na shahawa kwa mara ya kwanza ni dalili ya kuwa si mtoto tena, bali ana [[uwezo wa kuzaa]]: kwa hiyo awajibike kama [[mtu mzima]] kuhusu uwezo mpya aliojaliwa. Hasa azingatie kuwa uwezo wake huo bado ni mbichi: ingawa unaweza kusababisha mimba, mimba hiyo itaendelea kwa shida au kufa kabisa.
 
UbichiUbishi ni mkubwa zaidi upande wa [[nafsi]], kwa kuwa mvulana hajawa tayari kubeba mzigo wa [[familia]] mpya. Ndiyo sababu asichezee uwezo huo, bali ajiandae kuwa [[baba]] safi siku za mbele: ajipatie [[elimu]] au [[ufundi]] fulani, akomae kiutu na kutunza afya yake ya mwili na ya nafsi.
 
Msichana afanye vilevile aweze kuwa mama bora; kumbe akijiingiza mapema katika masuala ya [[ngono]], anahatarisha [[heshima]] yake pamoja na afya, kwa kuambukizwa maradhi yanayoweza yakasababisha [[utasa]] au kwa kuzaa kwa shida kabla ya wakati wa kufaa.
 
=== '''Nini kifanyike kwa mtu aliye balehe''' ===
* Kutojiingiza kwenye masuala ya ngono
 
* Kutoshirikiana na makundi maovu
* Kuepuka kukaa sehemu za gizani na kutokwenda sehemu [[hatarishi]]
* Kuzingatia usafi wa mwili na mavazi na hasa mavazi ya ndani
* Kupata elimu ya afya ya uzazi kutoka kwa wazazi au watu maalumu kama madaktari na wataalamu wengine wa masuala yahusuyo [[afya]] ya uzazi.
[[Jamii:Biolojia]]
[[Jamii:Saikolojia]]