Mfumo wa upumuaji : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 25:
 
===Oksijeni inayopatikana katika maji kutegemeana na halijoto===
Hapa nafasi ya kudumisha uhai inategemea na halijoto ya maji. Maji baridi huwa na oksijeni zaidi ndani yake kuliko maji ya vuguvugu. Maana maji baridi yenye sentigredi 0 °C yanashika miligramu 14.6 za oksijeni ndani ya kila lita ya maji matamu, lakini kwenye sentigredi 20 ni 9.1 mg/l na kwenye 30 °C ni 7.6 mg/l pekee.<ref>[http://www.engineeringtoolbox.com/oxygen-solubility-water-d_841.html Oxygen Solubility in Fresh and Sea Water]</ref> Katika maji ya chumvi kiwango ya oksijeni iko chini kwa sababu chumvi imechukua tayari sehemu ya uwezo wa maji ya kushika ndani yake dutu nyingine iliyoyeyushwa ndani yake.
 
Kwa hiyo samaki wengi wanapatikana pale ambako kuna maji baridi zaidi; wanyama wa maji wanaozoea maji baridi hawawezi kustawi katika maji ya moto zaidi maana wanakosa oksijeni waliozoea. [[Vituo vya umeme]] vinayoacha maji ya kupoza katika magimba ya maji ni hatari kwa sehemu kubwa ya uhai katika maji.