Beda Mheshimiwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 5:
Hasa anafahamika kwa kitabu chake “Historia ya kikanisa ya taifa la Waingereza” (kwa [[Kilatini]]: ''Historia ecclesiastica gentis Anglorum''). Akiona [[Kanisa]] lilivyozidi kustawi kati ya mataifa mapya, alipenda kuonyesha lisivyobanwa na [[ustaarabu]] mmoja, bali linakumbatia kila aina ya [[utamaduni]] ili kuikamilisha katika [[Kristo]].
 
Beda anawajibikaalichangia kwa kiasi kikubwa kwa uenezaji wa hesabu ya miaka [[baada ya Kristo]] kuzaliwa.
 
Mwaka [[1899]] alitangazwa na [[Papa Leo XIII]] kuwa [[mtakatifu]] na [[mwalimu wa Kanisa]].
Mstari 30:
Alipofikia miaka 19 tu, ([[692]] hivi), alipewa [[daraja takatifu]] ya [[ushemasi]], na alipofikia miaka 30 ([[702]] hivi) alipata [[upadrisho]].
 
[[Mtaalamu]] wa [[biolojia]] na [[historia]], lakini hasa [[teolojateolojia]], alifaulu kufanya [[Biblia]] ieleweke kwa urahisi kupitia mahubiri yake sahili iliyofuata mfano wa ma[[babu wa Kanisa]].
 
Alipata kuwa kati ya wasomi wakuu wa [[Karne za Kati]] za mwanzo, akifaidika na ma[[gombo]] mengi muhimu aliyoletewa na maabati wake kutoka [[safari]] zao nyingi za [[ng’ambo]].
Mstari 48:
[[Hotuba]] zake zilifaulu kuongoza waamini waadhimishe vema mafumbo ya imani na kuyatekeleza maishani, huku wakitarajia [[ujio wa pili]] wa [[Yesu]] ili kuingizwa naye katika [[liturujia ya mbinguni]].
 
Akifuata masisitizo ya mababu kama [[Ambrosi]], [[Augustino]] na [[Sirili wa Aleksandria]], alifundisha kwamba [[sakramenti]] hazimfanyi mtu “awe Mkristo tu, bali Kristo mwenyewe”. Kila anayepokea kwa imani [[Neno la Mungu]] kwa mfano wa [[Bikira Maria]] anaweza kumzaa Kristo upya. Na Kanisa, kila linapobatiza watu, linakuwa “[[Mama wa Mungu]]” kwa kuwazaa kwa njia ya [[Roho Mtakatifu]].
 
Alihimiza [[walei]] wawe na [[bidii]] katika kupata mafundisho ya [[dini]] na kuwashirikisha mapema [[watoto]] wao. Pia wasali mfululizo kwa kutolea matendo yao yote kama [[sadaka ya kiroho]] pamoja na Kristo.