Wamasoni : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
+masunia
historia
Mstari 1:
[[Picha:Square compasses.svg|thumb|[[Lebo]] ya Umasoni inahusiana na asili ya chama kati ya wajenzi.]]
[[Picha:Freimaurer Initiation.jpg|thumb|200px|[[Kuingizwa]] katika chama cha Wamasoni [[karne XVIII]]. Lengo la [[ibada]] hiyo ni kuachana na maisha ya awali kwa kuigiza [[kifo]] na [[kuzaliwa upya]] katika maisha ya wanachama.]]
'''Wamasoni''' (yaani '''Waashi''' vilevile '''Masunia'''; ''[[ing.]] Freemasons'') ni [[chama]] cha [[siri]] kinachodai kufuata [[maadili]] na kustawisha [[udugu]] kati ya watu huru.
 
Msingi wake ni [[agano]] kati ya wanachama kwa ajili ya kushirikiana ili kufikia malengo ya pamoja.
 
Wamasoni wanatamka rasmi kutokuwa na [[ubaguzi]] wowote kati yao na kwa wanaotaka kujiunga nao, kufuatana na taratibu zilizopangwa katika ''Katiba ya waashi huru'' ambayo iandikwailiandikwa na [[James Anderson]] mwaka [[1723]] na inakubaliwa na miundo yote ya Kimasoni duniani ingawa kati yake kuna tofauti kadhaa kadiri ya mazingira.
 
Asili ya chama hicho haijulikani kwa hakika, hasa kabla ya mwaka [[1650]]. Vilevile siri inayotawala maisha ya chama, hata kati ya ngazi mbalimbali za waliojiunga, inafanya iwe vigumu kuelewa malengo halisi na mbinu zinazotumika kuyafikia duniani kote.
 
Chama kinafanana na [[dini]] yenye [[madhehebu]] na [[ibada]], hata kumbi zake zinaitwa ma[[hekalu]]. [[Mungu]] anaitwa kawaida [[Msanii majengo mkuu]] wa [[ulimwengu]]. [[Kanisa Katoliki|Wakatoliki]] (na baadhi ya [[Wakristo]] wengine) hawaruhusiwi kujiunga na chama hicho.
 
==Asili ya Wamasoni==
[[Kanisa Katoliki|Wakatoliki]] (na baadhi ya [[Wakristo]] wengine) hawaruhusiwi kujiunga na chama hicho.
Asili ya Wamasoni ilikuwa katika jumiya ya waashi yaani mafundi waliojenga makanisa makubwa ya Ulaya wakati wa [[zama za kati]]. Wakati ule mafundi wa fani mbalimbali walipaswa kuwa wanachama wa jumuiya wa ufundi wao. Jumuiya hizi zilitunza elimu yao kama siri na wanachama walipaswa kuahidi kutunza siri za ufundi wao pamoja na siri za jumuiya. Wote walitakiwa kusaidiana. Wakati wa kupokelewa mwanachama mpya alitoa kiapo kilichofuata na viapo vingine baada ya kupanda ngazi katika ufundi wake. Jumuiya hizi mara nyingi walikuwa na salamu na maneno ya siri zilizosaidia kujtambulisha kama ndugu wa jumuiya wakati wa kufika katika mji mwingine. Katika jamii ya Ulaya ya zama za kati jumuiya zote za mafundi zilikuwa pia na tabia ya kidini; kila mwanachama alipaswa kuwa Mkristo <ref>Hii ilikuwa sababu muhimu ya kwamba Wayahudi wa Ulaya walizuiliwa kutekeleza kazi nyingi za kifundi maana hawakupokelewa katika jumuiya za mafundi</ref>; kwa kawaida kila jumuiya ilijiweka chini ya ulinzi wa mtakatifu fulani na kuanza mikutano yao kwa sala na ibada. Mfumo huu wa ufundi ulikwisha polepole.
 
Katika [[Uingereza]] jumuiya za waashi ziliendelea hata wakati ujenzi wa makanisa makubwa ulipungua na elimu ya ufundi ilisambazwa zaidi tangu kuwepo wa [[uchapaji]] vitabu. Waashi walianza kupokea wanachama wasiokuwa wajenzi lakini waliendelea kujiita "Waashi huru" (ing. Free Masons). Uhusiano kati ya jumuiya za waashi na Ukristo ilibadilika kutokana na [[matengenezo ya kiprotestanti]] kwa sababu viongozi wa Kiprotestant walijaribu kupiga marufuku jumuiya za mafundi zilizoendelea na ibada zenye tabia nyingi za ukatoliki kati yao. Hata hivyo jumuiya ya waashi ziliweza kuendelea kutokana na umuhimu wa ufudi wao. Maandamano kwenye siku za watakatifu yalizuiliwa.
 
Wakati wa [[zama za mwangaza]] fikra za falsafa mpya zilienea na jumuiya za waashi ziliwapa wanachama wao nafasi ya kujadili fikra hizi kwa uhuru zaidi kuliko jamii kwa jumla kwa sababu ya tabia ya kisiri ya mikutano yao. Hapa mawazo ya "dini ya kimantiki" yalitokea na kwa jumla waashi huru kati yao waliunda ibada zilizokazia maadili mema bila kutaja tena mafundisho ya Kikristo hasa. Wanachama walipaswa kukiri imani katika "roho mkuu" bila kutumia tena lugha ya kikristo au kukubali mafundisho ya kikanisa. Walilenga kuunganisha Wakristo wa madhehebu mbalimbali pamoja na watu waliokataa imani ya kidini yoyote.
 
Wanaendelea kutumia vyeo vya kale kwa wanachama. Mgeni anapokelewa kama mwanagenzi ''(apprentice)'', anaendelea kuwa fundi ''(fellow)'' na mwenyekiti au msimamzi wa jumuiya kwenye halai fulani huitwa gunge ''(master)''. Jumuiya zao za kimahali zinaitwa nyumba ''(lodge)''.
 
{{mbegu-dini}}