Wamasoni : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 16:
Katika [[Uingereza]] jumuiya za waashi ziliendelea hata wakati ujenzi wa makanisa makubwa ulipungua na elimu ya ufundi ilisambazwa zaidi tangu kuwepo wa [[uchapaji]] vitabu. Waashi walianza kupokea wanachama wasiokuwa wajenzi lakini waliendelea kujiita "Waashi huru" (ing. Free Masons). Uhusiano kati ya jumuiya za waashi na Ukristo ilibadilika kutokana na [[matengenezo ya kiprotestanti]] kwa sababu viongozi wa Kiprotestant walijaribu kupiga marufuku jumuiya za mafundi zilizoendelea na ibada zenye tabia nyingi za ukatoliki kati yao. Hata hivyo jumuiya ya waashi ziliweza kuendelea kutokana na umuhimu wa ufudi wao. Maandamano kwenye siku za watakatifu yalizuiliwa.
 
Wakati wa [[zama za mwangaza]] fikra za falsafa mpya zilienea na jumuiya za waashi ziliwapa wanachama wao nafasi ya kujadili fikra hizi kwa uhuru zaidi kuliko jamii kwa jumla kwa sababu ya tabia ya kisiri ya mikutano yao. Hapa mawazo ya "dini ya kimantiki" yalitokea na kwa jumla waashi huru kati yao waliunda ibada zilizokazia maadili mema bila kutaja tena mafundisho ya Kikristo hasa. Wanachama walipaswa kukiri imani katika "roho mkuu" bila kutumia tena lugha ya kikristo au kukubali mafundisho ya kikanisa. Walilenga kuunganisha Wakristo wa madhehebu mbalimbali pamoja na Wayahudi na watu waliokataa imani ya kidini yoyote.
 
Kutoka Uingereza Wamasoni walienea hadi Ulaya bara na pia Marekani, baadaye pia katika koloni.
 
Wanaendelea kutumia vyeo vya kale kwa wanachama. Mgeni anapokelewa kama mwanagenzi ''(apprentice)'', anaendelea kuwa fundi ''(fellow)'' na mwenyekiti au msimamzi wa jumuiya ya kieneo huitwa gunge ''(master)''. Jumuiya zao za kimahali zinaitwa nyumba ''(lodge)''.