Ukristo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 146:
 
Mwishoni mwa [[karne ya 1]] [[cheo]] cha "Askofu" kiliimarika sana, lakini pia vikundi vya Wakristo wenye vyeo maalumu vya [[utumishi]] vilianza kutokea. Pamoja na Askofu vyeo vya [[Kasisi]] na [[Shemasi]] vilikuwa kawaida. Ma[[shemasi wa kike]] walipatikana pia mwanzoni, lakini walipotea baadaye, kutokana na [[utamaduni]] uliokazia [[kipaumbele]] cha [[wanaume]].
 
Kuanzia mwaka [[100]] hivi Kanisa likaitwa "[[katoliki]]" maana yake Kanisa moja kwa ajili ya nchi zote na watu wote, tofauti na vikundi vilivyojitenga nalo. Kila mji ulikuwa na askofu wake aliyeongoza kanisa. Maaskofu wa eneo au mkoa mmoja walikuwa chini ya [[Askofu Mkuu]]. Maaskofu wa [[Roma]] ([[Ulaya]] hadi Afrika Kaskazini-Magharibi), [[Aleksandria]] ([[Afrika]]) na [[Antiokia]] ([[Asia]]), waliheshimiwa kuliko maaskofu wengine wote wakaitwa "[[Papa]]" na "[[Patriarki]]". Cheo cha Patriarki kilipatikana pia kwa Askofu wa [[Bizanti]] (leo nchini [[Uturuki]]) baada ya ma[[kaisari]] wa Roma kuhamia kule, na vilevile kwa Askofu wa Yerusalemu.
 
Katika karne za baadaye vikundi mbalimbali vilianza kupinga kuwapo kwa vyeo maalumu vya utumishi. Walisisitiza zaidi "[[ukuhani]] wa Wakristo wote" maana yake kila Mkristo hushiriki utumishi ulio mmoja tu katika Kanisa. Madhehebu mengine ya Kiprotestanti, yakikumbuka sana matatizo ya utaratibu wa kiaskofu wakati wa [[karne za kati]], yaliona afadhali kuendelea bila cheo hicho. Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki pamoja na [[Wamoravian]] na [[Waanglikana]] wamehifadhi [[ngazi]] za kale yaani Uaskofu, Ukasisi na Ushemasi. Nchini [[Tanzania]] [[Walutheri]] pia [[Wabatisti]] wa aina ya A.I.C. wanaheshimu cheo cha Uaskofu. Lakini kimataifa sehemu kubwa ya Walutheri, na hasa [[Wapresbiteriani]] (Reformed) na Wabatisti hawana Askofu, wakisisitiza zaidi [[uwezo]] na [[haki]] ya kila Mkristo kushiriki katika shughuli zote za utumishi akichaguliwa.
Line 173 ⟶ 175:
Paulo ni mfano mzuri jinsi gani mtu aliyepinga Injili vikali aliongozwa kuihubiri. Nyaraka zake zinatuonyesha jinsi gani Mkristo anaweza kutumia [[akili]] yake pamoja na imani. Katika maandishi yake tunapata mtu aliyebebwa na imani katika matatizo na mateso makubwa. Anatufundisha kutoangalia Ukristo kama sheria au [[amri]] tu (Fanya! Acha!) bali kama jibu la [[upendo]] la mtu aliyeelewa upendo wa Mungu kwanza.
 
===Thoma====
Mtume anayekumbukwa sana kule [[India]] ni [[Mtume Thoma|Thoma]] (au: Tomaso) aliyefika mpaka Bara Hindi. [[Kaburi]] lake huonyeshwa katika mji wa [[Madras]]. Mpaka leo wako "Wakristo wa Thoma" kusini-magharibi mwa Bara Hindi. Kwa muda mrefu walikosa mawasiliano na Wakristo wengine waliokuwa mbali, lakini siku hizi wanashiriki katika [[umoja wa Kanisa]] duniani.