Radama I : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|upright|Mfalme [[Radama I (1810-1828)]] '''Mfalme Radama I''' (kuzaliwa 1792 - kufariki 18...'
 
No edit summary
 
Mstari 1:
[[Picha:Radama I, portrait by Ramanankirahina.gif|thumb|upright|Mfalme [[Radama I]], mfalme ([[1810]]-[[1828]]).]]
'''Mfalme Radama I''' (kuzaliwa [[1792]] - kufariki 1828) alirithi [[kiti cha ufalme]] cha [[Andrianampoinimerina]] katika [[kisiwa]] cha [[Madagaska]] mwaka [[1810]] akiwa na [[umri]] wa [[miaka 18]].
 
Jukumu lake la kwanza kabisa baada ya kushika [[ufalme wa Merina]] lilikuwa kuyapiga makundi ya ndani ya ufalme huo yaliyoasi.
 
Hata hivyo, mafanikio yake makubwa zaidi yalihusiana na upanuaji wa mipaka. Alitafuta [[njia]] moja kwa moja hadi [[bahari]]ni ili kufanikisha [[biashara]] baina yake na [[Wazungu]] na kuupanua [[utawala wa Merina]].
 
[[Jeshi]] lake si tu kuwa lilitumika kuyapiga [[majimbo]] mengine, bali pia kudumisha [[sheria]] na [[utulivu]] katika maeneo yaliyotekwa.
 
Hadi mwaka [[1825]], Radama alikwisha kuliteka eneo lote la [[pwani]] ya [[mashariki]] ya Bukini, kuanzia [[Vohema]] hadi [[ngome]] ya [[Dauphin]]. Aidha aliishinda sehemu kubwa ya [[magharibi]], ila ilikuwa vigumu kuiteka [[Sakalava]].
 
Pamoja na hayo yote, hadi mwaka [[1823]] Radama aliweza kuupanua utawala wa [[Merina]] katika sehemu kubwa sana ya kisiwa hicho.

Ingawa utawala wake katika kisiwa hicho chote haukukamilika, hakukuwa na kipingamizi chochote kikubwa dhidi ya kujitangaza kwake kuwa mfalme wa [[Bukini]].
 
Alifariki mwaka [[1828]] akiwa na umri wa miaka 36.