Biashara ya watumwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 8:
[[Uchumi]] wa [[Roma ya Kale]] ulitegemea watumwa waliokamatwa na kusafirishwa kutoka pande zote za [[mazingira]] ya [[Bahari Mediteranea]].
 
Milki za ma[[khalifa]] wa [[Uislamu]] ziliendelea kutegemea watumwa. [[Waosmani]] walichukua watoto wa [[Ukristo|Kikristo]], hasa kutoka nchi za [[Balkani]], na kuwapeleka kama watumwa katika sehemu za kusini za milki yao kama [[Misri]] walipofanya kazi kama [[wanajeshi]].

Biashara ya Waarabu kuhusu watumwa ilidumu miaka 1,300, na kupeleka mamilioni ya Waafrika, hasa [[wanawake]], upande wa [[Asia]].
 
Mahitaji ya uchumi wa kimataifa tangu [[karne ya 15]] yalisababisha kuongezeka kwa biashara ya watumwa hasa kutoka [[Afrika]]; mamilioni walikamatwa na watawala wa milki kwenye pwani za Afrika au [[Waarabu]] na kuuzwa kwa wafanyabiashara [[Wazungu]] waliowapeleka [[Amerika]] walipohitajika kwa kazi kwenye ma[[shamba]] makubwa ya [[miwa]] na [[pamba]].
 
Wareno na Wahispania waliunda utawala wao kule Amerika Kusini hasa katika [[karne ya 16]]. Walitafuta [[madini]] ya nchi hizo wakaanzisha mashamba makubwa. Lakini wakaona ugumu wa kutumia [[Wahindi wekundu]] kama wafanyakazi.
 
Watu hao waliishi miaka elfu kadhaa bila mawasiliano na watu wengine. Magonjwa yaliyokuwa kawaida Ulaya, Afrika na Asia (kwa sababu watu wa kule waliwahi kuambukizana tangu karne nyingi) yaliua wenyeji wengi wakiishi pamoja na [[Wazungu]]. Tena walowezi Wazungu walikuwa wakatili mno. Wahindi wekundu waliofanywa watumwa wakafa kwa mamilioni.
 
Hapo wazo jipya lilijitokeza: kuchukua watumwa kutoka Afrika ili wafanye kazi Amerika! Waliopendekeza wazo hili walisema Waafrika wana nguvu na [[afya]] kuliko wenyeji wa Amerika. Ndivyo ilivyotokea. Msingi wa maendeleo ya Ulaya uliwekwa kwa [[malighafi]] za Amerika zilizochimbwa na kulimwa na watumwa Waafrika.
 
Kwa karne tatu biashara ya watumwa ilikua na kuongezeka kwenye pwani za Afrika. Katika karne ya 16 Wareno walikuwa mstari wa mbele katika biashara hii ya aibu, halafu [[Waingereza]] wakashika nafasi ya kwanza kabisa wakauza watumwa popote.
 
Biashara hii ilianza kupingwa zaidi tangu mwisho wa [[karne ya 18]]; [[Mkutano wa Vienna]] ([[1814]]-[[1815]]) ulikuwa mapatano ya kwanza ya kimataifa yaliyolenga kukataza biashara ya watumwa kutoka Afrika.