Ukristo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 204:
 
Hiyo ilitokana na msimamo wa msingi wa [[urekebisho wa Kiprotestanti]] wa kutaka kila mmoja aweze kutafsiri [[Biblia]] alivyoielewa, bila kutegemea mapokeo wala [[mamlaka]] rasmi ya Kanisa, ila msaada wa Roho Mtakatifu.
 
[[Umoja]] halisi wa Kanisa unaweza kupatikana tu katika ukweli wa Injili ya Yesu Kristo. Ni habari mbaya kwamba katika [[karne ya 16]] kuupigania [[ukweli]] huo kulivunja umoja wa [[Ukristo wa magharibi]]. Haiwezekani kushangilia mafarakano ya wafuasi wa Yesu.
 
Yale ya karne hiyo yalitokana na kuelewa tofauti kweli za imani ya Kikristo na yalikuwa na ukali kwa sababu pande zote zilisadiki kwamba kushikilia kwa usahihi [[ufunuo]] wa Mungu ni suala la [[wokovu]] wa milele. Kwa mfano, [[Martin Luther]] aliandika,«Sikubali mafundisho yangu yahukumiwe na yeyote, hata kama ni malaika. Asiyekubali mafundisho yangu hawezi kufikia wokovu».<ref>Martin Luther, Weim., X, P. Il, 107, 8-11</ref>
 
Pamoja na hayo, mambo mengi yalichangia farakano, si [[teolojia]] tu, bali [[siasa]], [[uchumi]], [[jamii]] na [[utamaduni]]. Wakati huo mara nyingi [[hoja]] za imani na malengo ya kisiasa vilichanganyikana: wanasiasa wengi walitumia hoja hizo ili kufikia malengo ya kiutawala, na vilevile [[wanateolojia]] walitumia siasa kutetea mafundisho yao ili kuvuta watu. Ndiyo sababu Luther alichorwa kama [[shujaa]] wa [[taifa]] la [[Ujerumani]].
 
Mara nyingi pande zote zilipotosha maana ya wapinzani na kuwachora vibaya wakivunja amri ya nane inayokataza [[uongo]] dhidi ya jirani. Hata waliojitahidi kusema ukweli tu juu ya wengine kwa kawaida hawakujitahidi vya kutosha kuelewa msimamo wao na kuona kwamba pengine si mbaya zaidi. Kila mmoja alitaka [[ushindi]] akachangia [[ugomvi]] uliorithishwa kwa vizazi vilivyofuata.
 
Hivyo, kilichosababisha zaidi farakano si masuala ya imani yaliyojadiliwa na Waprotestanti, bali [[lawama]] zao dhidi ya hali mbaya ya Kanisa la wakati huo iliyokuwa inakera wengi na kuwaelekeza kuunga mkono [[urekebisho]].
 
Hapo kale neno hilo (kwa Kilatini reformatio) lilihusu badiliko la hali mbaya iliyopo ili kurudia hali nzuri zaidi ya awali. Katika [[Karne za Kati]] lilitumika mara nyingi kwa marekebisho ya [[umonaki]]. Katika [[karne ya 15]] haja ya urekebisho ilionekana wazi si tu kwa mashirika ya kitawa bali kwa Kanisa lote. Hasa [[Mtaguso wa Konstanz]] ([[1414]]-[[1418]]) ulidai kabisa ufanyike «katika [[kichwa]] na katika [[viungo]]». Lakini kwa jumla mitaguso yote ya Karne za Kati na mikutano mingi ya [[Bunge]] la [[Dola la Ujerumani]] ililenga urekebisho wa Kanisa.
 
Kwa kweli Karne za Kati zilikuwa na mchanganyiko wa mambo yaliyopingana: [[ibada]] za nje tu na za dhati kabisa; [[teolojia]] iliyoelekeza kutenda kwa msingi wa nipe nikupe na hakika ya kwamba [[binadamu]] anategemea kabisa [[neema]] ya Mungu; kutojali [[wajibu]] hata upande wa viongozi wa Kanisa na marekebisho safi ya mashirika ya kitawa.
 
[[Karne ya 15]] ilikuwa kipindi cha [[umotomoto]] wa pekee katika Kanisa, ambapo [[walei]] wengi zaidi na zaidi walipata elimu nzuri, hivyo walitamani [[hotuba]] bora na mafundisho ya kuwasaidia kuishi Kikristo zaidi. Luther aliitikia haja hizo zilizomgusa sana kama mtu wa wakati wake.
 
Luther alitumia kwa nadra neno urekebisho, lakini likaja kuwa jina la kawaida la matukio yale mengi ya miaka [[1517]] - [[1555]], yaani kuanzia uenezi wa [[hoja 95]] za Martin Luther hadi [[amani ya Augsburg]]. Kati yake chanzo, yaani mabishano ya Kikanisa yaliyosababishwa na teolojia ya Luther, yalichanganyikana mapema na siasa, uchumi na utamaduni, kutokana na hali halisi ya wakati huo, mbali kuliko mwenyewe alivyofikiri.
 
Tangu mwaka [[1907]] tapo la [[Wapentekoste]] limeenea duniani kote (linakadiriwa kuwa na waumini milioni karibu 300) na kuathiri hata madhehebu yote ya zamani (ambapo mara nyingi waumini wa aina hiyo wanaitwa "[[Wakarismatiki]]").