Calvin : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 28:
 
==Tathmini==
Tofauti na Luther, Calvin alijaribu moja kwa moja kujenga [[kanisa]] jipya kwenye msingi wa [[Biblia]].
 
Hakupenda kuchukua [[urithi]] wowote wa [[Kanisa Katoliki]], akaunda kila kitu upya kufuatana na jinsi alivyoelewa Biblia.
 
Katika [[utawala]] alikataa [[cheo]] cha [[uaskofu]] akaona kanisa liongozwe na [[Mzee|wazee]] wa kuchaguliwa. Kutokana na neno wazee katika [[lugha]] ya [[Agano Jipya]] ([[Kigiriki]]) "presbyuteroi", kanisa lake linaitwa pia la "Wapresbiteri". Wafuasi wake huitwa pia "Wareformati" (to reform = kutengeneza upya). Maana yake walikataa [[desturi]] zote wasizoziona katika Biblia, wakati Luther alizikubali zile alizoziona hazipingi Biblia.
 
Katika [[ibada]] zao, Wareformati wanakataa [[altari]], [[picha]] za kupamba kanisa au kuimba [[liturujia]], wakati ibada ya Kilutheri ni [[Misa]] ya Kikatoliki iliyobadilishwa kufuatana na mawazo ya Luther. Katika jambo hilo hawakupatana na ndiyo sababu kwa muda mrefu Walutheri na Wareformati walishindwa kuwa na ibada za pamoja, lakini siku hizi wanaelewana.
 
Mafundisho hayo kutoka Uswisi yalienea katika nchi kama [[Ufaransa]], [[Uskoti]] na [[Uholanzi]]. Hata [[Wamoravia]] walichukua sehemu ya mafundisho ya Wareformati, hasa juu ya [[Chakula cha Bwana]], wakimfuata Luther katika mambo mengine.
 
[[Afrika Kusini]] urithi wa kidini wa [[Makaburu]] ni wa Kireformati kwa sababu [[babu]] zao walitokawalitokea Uholanzi na Ufaransa.
 
Vilevile ni [[wamisionari]] kutoka Uswisi na Uskoti walioanzisha mapema makanisa ya Kipresbiteri [[Malawi]], [[Kenya]] na [[Afrika Magharibi]].
 
== Tanbihi ==