Waanabaptisti : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|Uenezi wa tapo hili katika [[Ulaya ya Kati miaka 1525-1550.]] {{Ukristo}} '''Waanabaptisti''' (kw...'
 
No edit summary
Mstari 8:
 
Kwa sasa Waanabaptisti wote hawafikii milioni 2 duniani.
 
==Historia==
Wakati wa [[Martin Luther]] yalianza pia [[madhehebu]] ambayo zamani hizo yalikataliwa na makanisa mengine yote: Waanabaptisti. Ni kwamba wakati ule wa mabadiliko walijitokeza [[Wakristo]] waliopenda kuwa karibu zaidi na mfano wa Ukristo wa kwanza. Walitaka Kanisa liwe jumuiya ya [[watakatifu]], yaani Wakristo wa kweli tu. Waliona wengi kuwa Wakristo wa jina tu.
 
Walivyojisomea Biblia walishindwa kuelewa [[desturi]] ya kubatiza watoto. Jinsi walivyoona, mwanzoni watoto wadogo hawakubatizwa ila watu wazima walioamini. Kwa jumla wakaona desturi ya kubatiza watoto wasiofahamu [[imani]] ni msingi wa kuwa na [[wanafiki]] na Wakristo wa uongo ndani ya kanisa.
 
Mwaka [[1525]] huko [[Uswisi]] ulitokea ubatizo wa mtu mzima. Aliwahi kubatizwa utotoni lakini alianza kuelewa imani na kuongoka katika umri mkubwa tu. Akajisikia apokee "ubatizo wa imani".
 
Habari hii na mafundisho yaliyolingana nayo vilienea haraka sana Uswisi na [[Ujerumani]]. Katika miji mbalimbali Wakristo walivutiwa kukutana katika vikundi vidogo nje ya makanisa, wakisali pamoja na kuwa na [[Chakula cha Bwana]] [[nyumba|nyumbani]] mwao. Walioamini kwa njia hiyo mpya walitafuta "ubatizo wa imani".
 
Viongozi [[Wakatoliki]] na pia [[Waprotestanti]] wakapinga mafundisho yao. Wakaona ni kudharau [[sakramenti]] ya ubatizo, maana wale wote wameshawahi kubatizwa kama watoto wadogo. Tena walikuwa na [[shaka]] juu ya kanisa kuwa [[jumuiya]] ya "Wakristo wa kweli tu". Nani aamue juu ya [[ukweli]] wa [[roho|rohoni]] kama si [[Mungu]] mwenyewe?
 
Jinsi Waanabaptisti walivyojaribu kulinda utakatifu wa kanisa lao kwa kuweka [[sharti|masharti]] mbalimbali juu ya [[maadili]], wengine waliona wameunda taratibu za [[binadamu|kibinadamu]]. Luther, aliyetoka katika [[jitihada]] za [[umonaki]] alipojaribu kujenga utakatifu wake kwa kutimiza masharti mengi, aliona kosa lilelile katika "watakatifu" wale.
 
Tatizo lingine lilikuwa uhusiano wao na [[serikali]] na [[dola]]. Walisoma katika Biblia kwamba Mkristo [[kiapo|asiape]] wala kutumia [[silaha]], wala kushiriki katika mambo ya serikali. Kumbe wakaonekana ni maadui wa kila serikali.
 
Jambo la kusikitisha sana ni kwamba madhehebu makubwa yaliyoendelea chini ya ulinzi wa serikali za maeneo yao yalikuwa tayari kuwagandamiza kinyama Waanabaptisti. Waliobatiza watu wazima na kuhubiri imani hiyo wakatafutwa na kukamatwa, kufungwa [[gereza|gerezani]] na hata kuuawa. Katika matendo ya namna hiyo zilishirikiana serikali zote za Ulaya, kama ni za Kikatoliki, za Kilutheri au za [[Wakalvini|Kikalvini]].
 
Baada ya wengi wao kuuawa, Waanabaptisti wengine walianza kujificha au kuhamia mahali walipopata ustahimilivu. Kikundi kimoja kiliweza kuishi [[Uholanzi]] na Ujerumani Kaskazini. Kiongozi wao alikuwa [[Menno Simoni]]. Wafuasi wake wakaitwa "Wamenno".
 
Baadaye wakahamia mpaka [[Urusi]] kutafuta mahali penye [[uhuru wa dini]] wasipolazimishwa kuwa [[wanajeshi]] wala kuapa [[mahakama|mahakamani]].
 
Walienea hasa [[Marekani]] walipokimbilia wafuasi wake kutoka sehemu mbalimbali za [[Ulaya]].
 
Katika [[karne]] zilizofuata [[wamisionari]] wao walirudi tena Ulaya na kuenea sehemu nyingine za [[dunia]].
 
Waanabaptisti wanaangalia zaidi [[uhuru]] wa ushirika pale wanaposali kuliko [[umoja wa Kanisa]], hivyo wako duniani katika vikundi mbalimbali.
 
Jumuiya zao zilipokua baadaye, sehemu kubwa ya Waanabaptisti waliacha tena masharti ya kutotumia silaha au kukataa kiapo mahakamani, kama tumeshaona katika vikundi vingine.
 
Nchini [[Tanzania]] Wamenno wako hasa [[kaskazini]], lakini kitovu cha Kanisa la Kibatisti lililoundwa na wamisionari Wamarekani ni katika [[Nyanda za Juu za Kusini]]. Kanisa la "[[African Inland Church]] - AIC" linafuata pia mapokeo ya Kibatisti katika mengi ila linatumia [[cheo]] cha [[Askofu]].
 
==Tanbihi==