Waluguru : Tofauti kati ya masahihisho
maudhui
(maneno kadhaa na ujumbe) |
(maudhui) |
||
'''Waluguru''' ni kabila la [[Tanzania]] wanaoishi katika mikoa ya [[Mkoa wa Morogoro|Morogoro]] na [[Mkoa wa Pwani|Pwani]], hasa kwenye [[Milima ya Uluguru]] ([[Wilaya ya Mvomero]]) na katika [[wilaya ya Morogoro vijijini]] ukianzia [[Matombo]] kuelekea [[Dutumi]] hadi [[Bwakila Juu]]. Kuna makundi makubwa mawili ya Waluguru. Makundi hayo ni Waluguru wanaoishi milimani na wale wanaoishi mabondeni. Waluguru wa milimani wanapatikana katika maeneo ya Mgeta, Kolero,baadhi ya maeneo ya Matombo na Kiroka, na pembezoni mwa Milima ya Uluguru hasa ile ya Tao la Mashakiri. Katika mfumo wa kifamilia Waluguru hufuata ukoo kwa mama yaani kwa kiingereza <nowiki>''</nowiki>matrilineare<nowiki>''</nowiki>. Hatahivyo, mtoto wa kiluguru huitwa jina la ukoo wa baba yake. Yaani: Waluguru wana 'mtala' na ukoo. Mtala ni jina la ukoo wa baba ambalo ndilo analoitwa mtoto. Kwa mfano: mtoto akiitwa 'Kobero' jina hili ni mtala na si la ukoo wake kwani 'kobero' ni jina analopewa mtoto ambaye baba yake ni 'mmadze'. Halikadhalika, mtoto akiitwa 'Mkude' jina hili ni mtala wa ukoo wa 'Wamwenda' lakini si la ukoo wa mtoto. Hivyo basi, kwa Waluguru baba hutao jina na mama hutoa ukoo: jina ni la ukoo wa baba, na ukoo ni wa mama!
Waluguru ni maarufu kwa kilimo cha magimbi na wana aina kadhaa za magimbi. Auna moja wapo ni ile ya 'mahimbi' ambayo huchukua muda mrefu kuiva. Iwapo aina hii ya mahimbi italiwa mapema kabla ya kuiva kabisa mlaji atawashwa midomo na ulimi. Hivyo basi, mpishi hupaswa kuwa mvumilivu kwa masaa kadhaa kabla ya kuepua chungu cha mahimbi na kuyala. Masuala ya jando na unyago yalikuwa ya kawaida sana kabla ya miaka ya tisini. Hatahivyo, maingiliano ya kijamii na kupanuka kwa elimu kumefanya shughuli hizi zisipewe kipaumbele. Waluguru wa milimani ni wahanga wa masimulizi ya "mumiani" kiasi kwamba mpaka sasa huweza kuwahusisha wageni na hao "mumiani".
Kielimu jamii hii haitilii maanani sana suala la elimu na ndio mana idadi kubwa ya watu wa jamii ya waluguru hawana elimu ya kutosha.
Waluguru wanapenda kuishi pamoja na kushirikiana. Pia hupensda kunywa pombe na kushiriki kwenye sherehe za kimila.
|