Open main menu

Changes

299 bytes added ,  miaka 3 iliyopita
no edit summary
[[Chama]] cha [[Afro-Shirazi Party]] (ASP), kilichowakilisha hasa Waafrika, kilipoona kwamba [[bunge|bungeni]] kina viti vichache ingawa kilipata 54% za [[kura]] katika uchaguzi wa Julai [[1963]], kilipatana na chama cha mrengo wa kushoto [[Umma Party (Zanzibar)|Umma Party]].
 
Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP [[John Okello]] ([[1937]]-[[1971]] ?) kutoka [[Uganda]] aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa [[kisiwa]] kikuu cha [[Unguja]] kushinda [[polisi]] wa nchi na kuteka [[silaha]] zao. Halafu walielekea [[Zanzibar Town]] walipompindua Sultani [[Jamshid bin Abdullah]] na serikali yake. Waliokufa katika mapigano wamekadiriwa kuwa 80 hivi tu.
 
YalifuataKumbe yalifuata kwa siku kadhaa (labda hadi tarehe [[20 Januari]]) [[maangamizi ya kimbari]] dhidi ya Waarabu (waliokuwa 50,000 hivi) na [[Waasia]] wa [[Asia Kusini]] (waliokuwa 20,000 hivi); hakuna hakika kulikokuhusu [[idadi]] ya waliouawa: [[kadirio|makadirio]] yanataja kuanzia mamia kadhaa hadi 20,000.
 
Kiongozi wa ASP [[Abeid Karume]], asiyekuwa na [[Itikadi kali|msimamo mkali]] akawa [[rais]] wa kwanza wa nchi, na wanachama wa Umma party walipewa nafasi serikalini. Kufikia Machi Okello alikuwa ameshawekwa pembeni na kufikia Aprili kikosi chake kimeshanyang'anywa silaha.
 
Mwelekeo wa [[Ukomunisti|Kikomunisti]] wa baadhi katika serikali mpya uliogopesha [[nchi za Magharibi]]. Kwa kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya athari ya Uingereza, serikali yake iliandaa mipango kadhaa. Hata hivyo, hofu ya kuundwa serikali ya Kikomunisti haikutimia kamwe, na kwa kuwa wananchi wa Uingereza na [[Marekani]] waliweza kuhama bila shida, mipango hiyo haikutekelezwa.
 
Wakati huo [[nchi za Kikomunisti]] za [[China]], [[Ujerumani Mashariki]] na [[Umoja wa Kisovyeti]] zilianzisha mahusiano ya kirafiki na serikali mpya ya Zanzibar kwa kuitambua rasmi na kwa kutuma washauri.