Jamhuri ya Watu wa China : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 139:
Zaidi ya [[asilimia]] 90 za wakazi wote wanakaa katika [[theluthi]] ya kusini-mashariki ya nchi yenye mvua ya kutosha. Ndani ya theluthi hiyo ni nusu ya Wachina wote wanaosongamana kwenye asilimia 10 za China yote, maana yake katika 10% hizi kuna msongamano wa watu 740 kwa km².
 
Wakazi walio wengi ni [[Wahan]] au Wachina wenyewe. Wanatumia hasa [[lahaja]] mbalimbali za [[lugha]] ya [[Kichina]]. Pamoja na Wahan kuna ma[[kabila]] 55 yaliyotambuliwa na [[serikali]]. Kwa jumla [[lugha hai]] ni 292 ambazo zinahusika na makundi mbalimbali ya lugha (angalia [[orodha ya lugha za China]]).
 
Serikali inafuata rasmi [[ukanamungu]], lakini inaruhusu [[dini]] kwa kiasi fulani. Pamoja na hayo, dhuluma zinaendelea dhidi ya [[madhehebu]] mbalimbali. Takwimu hazieleweki, pia kwa sababu kabla ya Ukomunisti kupinga dini, hasa wakati wa [[Mapinduzi ya utamaduni]], watu waliweza kuchanganya mafundisho na [[desturi]] za [[Ukonfusio]], [[Utao]] na [[Ubuddha]]. Leo wanaoendelea kufanya hivyo wanakadiriwa kuwa asilimia 30-80 za wakazi. Wabuddha ni 6-16%, [[Wakristo]] (hasa [[Waprotestanti]], halafu [[Wakatoliki]] na kidogo [[Waorthodoksi]]) ni 2-4%, [[Waislamu]] ni 1-2%.