Meksiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 71:
Kilimo kiliweka msingi kwa vijiji na jamii zilizishirikiana katika maeneo makubwa. Miji ya kwanza inajulikana kuanzia takriban mwaka 1,500 KK.
 
====Waolmeki====
Ustaarabu wa kwanza unaojulikana ulikuwa wa [[Waolmeki]] baina 1.500 na 400 KK. Habari zao zinajulikana kutokana na [[akiolojia]] na mabaki ya miji na sanaa yao. Waolmeki walijenga miji wakaacha mifano ya sanaa yenye kiwango cha juu. Waliishi katika kanda la pwani la Mexiko katika majimbo ya leo ya [[Veracruz (jimbo)|Veracruz]] na [[Tabasco (jimbo)|Tabasco]]. Ni watu wa kwanza katika Mexiko wanaojulikana kubuni [[mwandiko]] na [[kalenda]], mchezo wa [[mpira]] na ujenzi wa [[piramidi]] za hekalu. Walikuwa hodari sana kuchonga sanamu ya mawe, hasa vichwa vikubwa vyenye urefu zaidi ya mita 3. Walifaulu kuunda sanaa hii bila kujua vifaa vya [[metali]]. Sanamu nyingine inayorudirudi ni mtu-jagwaa ibnayounganisha sehemu ya maumbile ya binadamu na [[jagwa]]. Takriban mwaka 400 - 300 KK miji yao iliachwa na wakazi hakuna uhakika ni nini iliyosababisha mwisho wa ustaarabu huu.
[[Picha:Zacuelu2.jpg|thumbnail|Hekalu - piramidi ya Kimaya]]
[[Picha:Madrid Codex 9.jpg|thumbnail|Ukurasa kutoka kitabu cha Kimaya - maandishi ya hiroglifi]]
====Wamaya====
Upande wa mashariki wa Waolmeki ustaarabu wa [[Wamaya]] ulianza tangu takriban mwaka 2,000 KK. Wamaya walikalia rasi ya [[Yucatan]] pamoja na Guatemala na Belize ya leo. Waliishi katika vijiji na miji iliyojitegemea na kugombana kati yao mara kwa mara. Wamaya walibuni mwandiko wa [[hiroglifi]] mwenye alama nyingi kupita maandishi mengine katika Amerika ya Kale na kutunga vitabu. Waliendeleza pia hisabati, wakijua namba "[[sifuri]]" na kuboresha mfumo wa kalenda. Walikuwa hodari sana katika [[astronomia]] yaani elimu ya nyota. Walipamba miji yao kwa majengo makubwa na mazuri na kuwa wafanyabiashara hodari. Sanaa yao ilijua uchongaji wa mawe na pia uchoraji.
 
== Watu ==