Mexiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 70:
[[Picha:20041229-Olmec Head (Museo Nacional de Antropología).jpg|250px|thumbnail|left|Sanamu ya kichwa ya Kiolmeki]]
Kilimo kiliweka msingi kwa vijiji na jamii zilizishirikiana katika maeneo makubwa. Miji ya kwanza inajulikana kuanzia takriban mwaka 1,500 KK.
 
Staarabu mbalimbali zilistawi na kukua katika maeneo ya pwani (Waolmeki, Wamaya) na katika nyanda za juu ya Mexico kati (Wazapoteki, Wamixeki, Watolteki, Waazteki).
 
====Waolmeki====
Ustaarabu wa kwanza unaojulikana ulikuwa wa [[Waolmeki]] baina 1.500 na 400 KK. Habari zao zinajulikana kutokana na [[akiolojia]] na mabaki ya miji na sanaa yao. Waolmeki walijenga miji wakaacha mifano ya sanaa yenye kiwango cha juu. Waliishi katika kanda la pwani la Mexiko katika majimbo ya leo ya [[Veracruz (jimbo)|Veracruz]] na [[Tabasco (jimbo)|Tabasco]]. Ni watu wa kwanza katika Mexiko wanaojulikana kubuni [[mwandiko]] na [[kalenda]], mchezo wa [[mpira]] na ujenzi wa [[piramidi]] za hekalu. Walikuwa hodari sana kuchonga sanamu ya mawe, hasa vichwa vikubwa vyenye urefu zaidi ya mita 3. Walifaulu kuunda sanaa hii bila kujua vifaa vya [[metali]]. [[Picha:Zacuelu2.jpg|thumbnail|Hekalu - piramidi ya Kimaya]]
[[Picha:Madrid Codex 9.jpg|thumbnail|150px|Ukurasa kutoka kitabu cha Kimaya - maandishi ya hiroglifi]]
Sanamu nyingine inayorudirudi ni mtu-jagwaa ibnayounganisha sehemu ya maumbile ya binadamu na [[jagwa]]. Takriban mwaka 400 - 300 KK miji yao iliachwa na wakazi hakuna uhakika ni nini iliyosababisha mwisho wa ustaarabu huu.
 
Line 80 ⟶ 82:
 
Jamii ya Wamaya ilifikia kiwango cha juu kuanzia mwaka 500 KK wakati miji mikubwa ya kwanza ilipotokea. Mnamo mwaka 800 BK jamii za Wamaya katika Yucatan ziliporomoka; wataalamu wengi huamini ya kwamba mabadiliko ya ekolojia na halihewa pamoja na kuchoka kwa utba ya ardhi yalisababisha kutoka kwa watu katika makazi ya awali. Lakini ustaarabu huu uliona tena kipindi cha kustawi katika maeneo mengine hadi kuja kwa Wahispania. Miji mbalimbali ya Wamaya iliendelea kujitetea dhidi ya wavamizi na Nojpeten , mji wa mwisho wa kujitegemea ulitekwa mwaka [[1696]].
 
==== Teotihuacan ====
[[Teotihuacan]] ilikuwa mji mkubwa katika nyanda za juu, karibu na Mexico City ya leo. Kuanzia mwaka 100 KK hadi takriban 550 BK ilikuwa mji mkubwa wa Amerika, pia moja kati ya miji mikubwa duniani na kitovu cha utamaduni kilichoathiri staarabu zote za Mexiko. "Teotihuacan" ilikuwa jina la Waazteki kwa mji huu, jina la kienyeji halikuhifadhiwa. Maana ya jina ni "mahali pa kuzaliwa kwa miungu". Wakati wa maendeleo yake mji ulikuwa na eneo la kilomita za mraba 30 ukiwa na wakazi angalau 150,000, labda hata 250,000 walioishi humo<ref>[http://www.dartmouth.edu/~izapa/M-15.pdf Architecture, Astronomy, and Calendrics in Pre- Columbian Mesoamerica, Vincent H. Malmstrom ]</ref>.
 
Hakuna uhakika ni akina nani waliojenga Teotohuacan. Mji wote ulipangwa kwa kufuata barabara mbili zilizoelekea kaskazini-kusini na mashariki-magharibi. Hekalu kubwa na piramidi zinaonyesha umuhimu wa dini, na mabaki ya nyumba za wakubwa na watu wa kawaida yanaruhusu kupata picha ya jamii iliyoishi hapa. Teotohuacan ilikuwa kitovu cha biashara ya misafara ya mbali na pia ya elimu. Ukubwa wa mji unaonyesha kiwango cha juu cha utawala na ushirikiano kati ya watu wake.
 
Katika karne ya 6 BK sehemu kubwa ya majengo iliharibika na kuchomwa. Hakuna uhakika kama hii ilikuwa tokeo la uvamizi kutoka nje au mvurugo au mapinduzi ndani ya mji. Baada ya maharibio yale mji ulianza kurudi nyuma na idadi ya watu kupungua. Mnamo mwaka 750 BK watu wote waliondoka ni maghofu ya majengo makubwa tu yaliyobaki<ref>[http://www.metmuseum.org/toah/hd/teot/hd_teot.htm Teotihuacan, Department of Arts of Africa, Oceania, and the Americas, The Metropolitan Museum of Art October 2001]</ref>.
 
[[Picha:View from Pyramide de la luna.jpg|thumbnail|Barabara ya mahekalu na piramidi ya jua mjini Teotihuacan]]
 
== Watu ==