Meksiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 84:
 
==== Teotihuacan ====
[[Picha:View from Pyramide de la luna.jpg|thumbnail|Barabara ya mahekalu na piramidi ya jua mjini Teotihuacan]]
 
[[Teotihuacan]] ilikuwa mji mkubwa katika nyanda za juu, karibu na Mexico City ya leo. Kuanzia mwaka 100 KK hadi takriban 550 BK ilikuwa mji mkubwa wa Amerika, pia moja kati ya miji mikubwa duniani na kitovu cha utamaduni kilichoathiri staarabu zote za Mexiko. "Teotihuacan" ilikuwa jina la Waazteki kwa mji huu, jina la kienyeji halikuhifadhiwa. Maana ya jina ni "mahali pa kuzaliwa kwa miungu". Wakati wa maendeleo yake mji ulikuwa na eneo la kilomita za mraba 30 ukiwa na wakazi angalau 150,000, labda hata 250,000 walioishi humo<ref>[http://www.dartmouth.edu/~izapa/M-15.pdf Architecture, Astronomy, and Calendrics in Pre- Columbian Mesoamerica, Vincent H. Malmstrom ]</ref>.
 
Hakuna uhakika ni akina nani waliojenga Teotohuacan. Mji wote ulipangwa kwa kufuata barabara mbili zilizoelekea kaskazini-kusini na mashariki-magharibi. Hekalu kubwa na piramidi zinaonyesha umuhimu wa dini, na mabaki ya nyumba za wakubwa na watu wa kawaida yanaruhusu kupata picha ya jamii iliyoishi hapa. Teotohuacan ilikuwa kitovu cha biashara ya misafara ya mbali na pia ya elimu. Ukubwa wa mji unaonyesha kiwango cha juu cha utawala na ushirikiano kati ya watu wake.
 
Katika karne ya 6 BK sehemu kubwa ya majengo iliharibika na kuchomwa. Hakuna uhakika kama hii ilikuwa tokeo la uvamizi kutoka nje au mvurugo au mapinduzi ndani ya mji. Baada ya maharibio yale mji ulianza kurudi nyuma na idadi ya watu kupungua. Mnamo mwaka 750 BK watu wote waliondoka ni maghofu ya majengo makubwa tu yaliyobaki<ref>[http://www.metmuseum.org/toah/hd/teot/hd_teot.htm Teotihuacan, Department of Arts of Africa, Oceania, and the Americas, The Metropolitan Museum of Art October 2001]</ref>.
 
[[Picha:View from Pyramide de la luna.jpg|thumbnail|Barabara ya mahekalu na piramidi ya jua mjini Teotihuacan]]
 
== Watu ==