Makaburu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Tengua pitio 970283 lililoandikwa na Aliwal2012 (Majadiliano)
Mstari 3:
Wako takriban theluthi mbili ya wazungu wa Afrika Kusini au milioni 1.5. Karibu wote ni Wakristo Waprotestanti hasa wa madhehebu ya Kikalvini.
 
Baada ya kushindwa katika [[vita ya pili ya Makaburu dhidi ya Uingereza]] mwaka 1902 na pia baada ya mwisho wa apartheid vikundi vya makaburu walihamia nje ya nchi kwenda nchi nyingine za Afrika na pia za Amerika.
 
==Historia==
Mababu zao ni mchanganyiko wa wahamiaji kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani, waliofika tangu mwaka 1652 katika koloni ya [[Kampuni ya Kiholanzi ya India ya Mashariki]]. Walikaa huko kama wakulima waliouza mazao kwa meli zilizozunguka kati ya Uholanzi na koloni za kampuni katika [[Indonesia]] ya leo. Mwaka 1814 ambako Uingereza ilitwaa utawala juu ya [[Koloni ya Rasi]] na hapo sehemu ya makaburu walianza kuondoka katika eneo la koloni na kuingia katika nchi upande wa kaskazini walipounda jamhuri zao kama [[Transvaal]], [[Dola Huru la Oranje]] na [[Natalia]]. Hasa kufutwa kwa utumwa mwaka 1834, sheria ya kufanya Kiingereza lugha rasmi na matumizi ya sheria za Uingereza zilisababisha kuondoka kwa Makaburu wengi katika koloni ya Rasi waliojulikana kama [[Voortrekker]].
 
Jamhuri za makaburu zilitwaliwa polepole na Waingereza waliowafuata. Jamhuri ya Transvaal ilitambuliwa na Uingereza mara ya kwanza mwaka 1852; ilitwaliwa 1877 lakini baada ya [[vita ya kwanza ya makaburu dhidi ya Uingereza]] uhuru wake ulitambuliwa tena. Waziri mkuu wa serikali ya koloni ya Rasi Cecil Rhodes alikuwa adui wa uhuru wa makaburu na baada ya kupatikana kwa almasi katika eneo la Johannesburg alijaribu kupindua serikali ya Transvaal. hii ilisababisha [[vita ya pili ya Makaburu dhidi ya Uingereza]]. Waingereza walishinda na katika [[amani ya Vereeniging]] makaburu walipaswa kukubali ubwana wa Uingereza. Lakini miaka kadhaa baadaye Uingereza uliwapa makaburu haki ya kujitawala katika mambo ya ndani.
 
1910 maeneo ya Kiingereza pamoja na majimbo ya Makaburu yaliungana kuwa [[Muungano wa Afrika Kusini]]. Hapo lugha ya [[Kiholanzi]] (lugha mama ya Kiafrikaans) ilitambuliwa kama lugha rasmi ya nchi pamoja na Kiingereza. 1925 Kiafrikaans ilikubaliwa kama lugha rasmi badala ya Kiholanzi.
Mstari 18:
== Tazama pia ==
* [[Kiafrikaans]]
* [[Natalia]]
* [[Dola Huru la Orange]]
* [[Transvaal]]
* [[Voortrekker]]