Meksiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 108:
 
Katika [[karne ya 6]] BK sehemu kubwa ya majengo iliharibika na kuchomwa. Hakuna uhakika kama hii ilikuwa tokeo la uvamizi kutoka nje au vurugu au [[mapinduzi]] ndani ya mji. Baada ya maharibio yale mji ulianza kurudi nyuma na idadi ya watu kupungua. Mnamo mwaka [[750]] BK watu wote waliondoka: ni [[ghofu|maghofu]] ya majengo makubwa tu yaliyobaki<ref>[http://www.metmuseum.org/toah/hd/teot/hd_teot.htm Teotihuacan, Department of Arts of Africa, Oceania, and the Americas, The Metropolitan Museum of Art October 2001]</ref>.
 
====Milki ya Azteki====
Kuanzia mwaka 1325 kabila la [[Azteki]] likaunda mji wa [[Tenochtitlan]] kwenye kisiwa cha [[ziwa la Tezcoco]]. Waazteki wakaendelea kuunda milki kubwa lililoeena na kutawala sehmu kubwa ya nyanda za juu za Mexiko. Msingi wa milki yao ilikuwa ushirikiano na mji miwili jirani iliyounda mwungano wa pande tatu lakini Waazteki waliendelea kuwa mshiriki mkuu na mtawala wa Tenochtitlan hatimaye alikuwa mtawala mkuu. Walishambulia maeneo ya miji na makabila jirani na kuwalazimisha kulipa kadi kwao. Kama walikubali kutoa kodi kila mwaka na pia kushiriki katika vita za milki watawala wa kienyeji waliruhusiwa kuendelea na utawala wa ndani. Dini yao iliweka uzito kwa sadaka za binadamu waliochinjwa kwenye mahekalu ya miungu yao. Waliunda mfumo wa mikataba ya vita na milki nyingine ambako walikutana kwa mapigano yaliyo kubaliwa awali kwa shabaha ya kukamata wafungwa wengi iwezekanavyo na kuwatoa kama sadaka kwa miungu hekaluni baadaye.
 
====Uvamizi wa Wahispania====
Mwaka 1519 Mhispania [[Hernan Cortez]] alifika kwenye pwani la Mexiko. Katika miaka iliyofuata alifaulu kuendelea hadi mji wa Tenochtitlan akiongozana na kundi la Wahispania mamia kadhaa. Cortez aliweza kuungana na miji na makabila ya Waindio waliochoka utawala wa Azteki na kumpa askari za usaidizi. Mwaka 1520 waliingia Tenochtitlan kama wageni wa mfalme [[Montezuma II]] wakaendelea kumkamata lakini baada ya kifo cha mfalme walifukuzwa wakakimbia kwa matatizo katika "usiku wa huzuni" (Kihisp. ''noche triste''). Waazteki walidhoofishwa sana kutokana na [[epidemia]] ya ugonjwa wa [[ndui]]<ref>Ndui ilikuwa ugonjwa iliyokuwa kawaida katika Ulaya wakati ule lakini ilikuwa ugonjwa mgeni kwa wenyeji wa Amerika ambao walikosa kinga dhidi yake; hivyo ilikuwa kati ya magonjwa wa kuambukizwa kutoka Ulaya yaiyoua Waindio wengi katika karne zilizofuata.</ref>. Cortez aliweza kukusanya jeshi kubwa la Waindio waliopinga Waazteki akavamia na kuharibu Tenochtitlan mwaka 1521 na kwenye magofu ya mji huu alianzisha mji mpya wa [[Mexico City]] (Kihisp. ''Ciudad de Mexico'').
 
===Ukoloni===