Mexiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 110:
 
====Milki ya Azteki====
[[Picha:Tlacochcalcatl.jpg|thumbnail|Askari wa Azteki]]
Kuanzia mwaka 1325 kabila la [[Azteki]] likaunda mji wa [[Tenochtitlan]] kwenye kisiwa cha [[ziwa la Tezcoco]]. Waazteki wakaendelea kuunda milki kubwa lililoeena na kutawala sehmu kubwa ya nyanda za juu za Mexiko. Msingi wa milki yao ilikuwa ushirikiano na mji miwili jirani iliyounda mwungano wa pande tatu lakini Waazteki waliendelea kuwa mshiriki mkuu na mtawala wa Tenochtitlan hatimaye alikuwa mtawala mkuu. Walishambulia maeneo ya miji na makabila jirani na kuwalazimisha kulipa kadi kwao. Kama walikubali kutoa kodi kila mwaka na pia kushiriki katika vita za milki watawala wa kienyeji waliruhusiwa kuendelea na utawala wa ndani. Dini yao iliweka uzito kwa sadaka za binadamu waliochinjwa kwenye mahekalu ya miungu yao. Waliunda mfumo wa mikataba ya vita na milki nyingine ambako walikutana kwa mapigano yaliyo kubaliwa awali kwa shabaha ya kukamata wafungwa wengi iwezekanavyo na kuwatoa kama sadaka kwa miungu hekaluni baadaye.