Mexiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 124:
===Tangu uhuru hadi leo===
Baada ya [[karne]] tatu na baada ya [[vita]] vya [[ukombozi]], mwaka 1821 wakazi walijipatia [[uhuru]] kwa jina la Mexico.
 
====Vita ya uhuru ====
Mfano wa uhuru wa Marekani mwaka [[1776]] ilikuwa na athira pia kati ya wasomi wenyeji wa Mexiko. Jamii ya kikoloni liliundwa juu ya ubaguzi kati ya Kreoli (wenyeji wenye asili ya Hispania bila mchanganyiko na Waindio), Mestizos (asilimia kubwa ya wenyeji waliotokana na ndoa za wanaume Wahispania na wake Waindio) na Waindio wenyewe. Lakini vyeo vyote vya juu kama maafisa wa juu wa serikali vilipatikana pekee kwa watu waliozaliwa Hispania na kutumwa Mexiko. Mawazo ya uhuru yalianza kupatikana kati ya Kreoli na Mestizos wa tabaka za juu.
 
Chanzo cha vita ya uhuru kilikuwa mabadiliko katika Ulaya. Napoleon mtawala wa Ufaransa alimkamata mfalme Ferdinand VII wa Hispania akamlazimisha kujiuzulu na kumpa kakaye Joseph Napoleon ufalme wa Hispania. Hatua hii ilifuatwa na wimbi la uasi nchini Hispania dhidi ya mfalme Mfaransa. Katika Hispania Mpya (Mexico) kamati za miji kadhaa zilizoongowa na Kreoli ziliapa kumfuata mfalme mfungwa halali pekee. Kamati Kuu ya Mexiko City ilitaka kuanzisha bunge la pekee kwa sababu Hispania haikuwa tena na serikali halali. Mfalme mdogo (gavana mkuu) alikubali. Viongozi wengine walitangaza ilhali mfalme halali hayuko tena sasa nguvu yote iko mkononi mwa wananchi. Hapo Wahispania katika koloni walioshika vyeo vikuu waliamua kumpindua mfalme mdogo na kuwakamata viongozi wa Kreoli. Uasi ulifaulu lakini vikundi vidogo vya wapinzani kwa uhuru kutoka Hispania waliendelea kukutana nchini na kukusanya viongozi. Hatimaye padre Kreoli [[Miguel Hidalgo y Costilla]] alikusanya jeshi la wanamigambo wakulima Waindio na Kreoli akapigana na jeshi lililokuwa chini ya mamlaka ya maofisa Wahispania. Miguel Hidalgo alishindwa na kuuawa lakini hii ilikuwa chanzo cha uasi mkubwa ambako Wakreoli na wakulima Waindio walipigana na jeshi lililofuata amri ya Wahispania katika koloni.
 
Mwaka kiongozi wa upande wa migambo ya uhuru Guerrero na jenerali wa jeshi la serikali Iturbide walikutana wakapatana kuungana. Vikosi vingi vya jeshi la kikoloni vilihamia upande wao. Gavana mpya aliyefika kutoka Hispania aliamua kukubali uhuru uliotangazwa tarehe 28 Septemba 1821.
 
 
 
 
Lakini miaka iliyofuata nchi haikupata msimamo kisiasa wala kiuchumi.