Eurasia : Tofauti kati ya masahihisho

ardhi ya bara inayojumuisha Ulaya na Asia
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'right|200px|thumbnail|Eneo la Eurasia Picha:Possible definitions of the boundary between Europe and Asia.png|300px|thumbnail|Nji...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:00, 2 Aprili 2016

Eurasia ni jina la kutaja nchi zote za Asia na Ulaya kwa pamoja. Jina hili linaunganisha maneno "Europa" na "Asia".

Eneo la Eurasia
Njia mbalimbali za kuchora mpaka kati ya Ulaya na Asia

Hali halisi Ulaya na Asia ziko pamoja kama nchi kavu mfululizo na hakuna bahari inayoyatenganisha. Kwa hiyo Ulaya na Asia haziitwa mabara kwa sababu za kijiografia lakini kwa sababu za kihistoria na kiutamaduni tu. Uzoefu huu unatokana na Wagiriki wa Kale waliokuwa watu wa kwanza wa kugawa dunia katika sehemu tatu tofauti (Ulaya, Asia na Afrika) na hivyo kuweka msingi kwa ugawaji wa dunia kwa mabara.

Wataalamu wengi wa jiografia wanaana ya kwamba masi ya nchi kavu inayojumlisha Ulaya na Asia ina tabia zote za bara moja na hivyo hutumia jina la "Eurasia".

Tangu kale swali la mpaka kati ya Ulaya na Asia lilikuwa tata na kuna majibu mbalimbali. Wengu hukubaliana ya kwamba msatri unafuata milangobahari ya Dardaneli na Bosporus (nchini Uturuki), mwambao wa Bahari Nyeusi na Bahari Kaspi halafu safu ya milima ya Ural hadi Bahari Aktiki. lakini kati ya bahari Nyeusi na kaspi katika eneo la Kaukasus mawazo hutofautiana sehemu gani ni ya Asia na zipi ya Ulaya.