Meksiko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 157:
Miaka hadi 1921 [[vita ya wenyewe kwa wenyewe]] iliharibu sehemu kubwa za nchi. Kuna makadirio ya kwamba wananchi milioni 1,5 (kati ya milioni 15) waliuawa na zaidi ya 200,000 walikuwa [[wakimbizi]], hasa kwenda Marekani<ref>[http://www.hist.umn.edu/~rmccaa/missmill/mxrev.htm Robert McCaa, "Missing millions: the human cost of the Mexican Revolution." Mexican Studies 19#2 (2001)]</ref>.
 
Mwaka [[1917]] katiba mpya ya nchi ilitolewa na mkutano wa bunge maalumu. Katiba hii ilikuwa katiba ya kwanza duniani kutangaza [[haki za kijamii]]. Hizo haki zililenga kutunza na kuboresha hali ya wananchi wenye maisha magumu kama wafanyakazi na wakulima dhidi ya [[ubepari|mabepari]] na wenye mashamba makubwa<ref>[https://books.google.com.mx/books?id=rwaNmEXho5QC&q=%22out+social+rights%22&hl=es-419#v=snippet&q=%22out%20social%20rights%22&f=false Akhtar Majeed, Ronald Lampman Watts, and Douglas Mitchell Brown (2006). Distribution of powers and responsibilities in federal countries. McGill-Queen's Press. p. 188. ISBN 0-7735-3004-5.]</ref>. Katiba hii iliweka mamlaka nyingi mikononi mwa rais wa taifa anayechaguliwa na wananchi wote kwa kipindi kimoja cha miaka 6, halafu hawezi kuchaguliwa tena. Shabaha nyingine ya vifungu katika katiba ilikuwa kupunguza uwezo wa Kanisa Katoliki kuathiri siasa na jamii na hatimaye kukomesha [[imani]] hiyo.
 
Siasa hii dhidi ya [[ukasisiUkristo]] iliendelea chini ya rais Calles na hatimaye kusababisha kipindi kingine cha vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya [[1926]]-[[1929]]. Katika mapigano hayo yaliyoitwa ''[[La Cristiada]]'' wakulima wengi walichukua silaha kwa jina la [[Kristo]] [[Kristo Mfalme|Mfalme]] dhidi ya jeshi la serikali ili kutetea [[uhuru wa dini]], wakipinga kufungwa kwa [[Kanisa|makanisa]], kuzuiwa [[ibada]] mbalimbali za hadhara na kuuawa kwa mapadre kama [[Mtakatifu]] [[Kristofa Magallanes]] na wenzake. Vita hivyo vilisababisha vifo 250,000 na idadi hiyohiyo ya wakimbizi waliojisalimisha Marekani.
 
Baada ya mapinduzi mamlaka ilichukuliwa na Chama cha kitaifa cha mapinduzi (Partido Nacional Revolucionario PNR) kilichoendelea kutawala kwa miaka 71 kuanzia 1929 hadi [[2000]].