Jalidi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Masahihisho
No edit summary
Mstari 4:
 
Mimea ya nchi ambako jalidi ni hali ya kawaida wakati wa majira ya baridi ina uwezo wa kukauka kabla ya majira ya jalidi kuanza. Katika mazingira ya joto mimea hufa mara nyingi kama baridi huwa kali.
 
Kama hali ya jalidi inaendelea kwa wiki mfululizo inaathiri pia ardhi yaani udongo. Ardhi yenyewe inaganda hadi kimo fulani kinachotegemea muda wa kudumu kwa jalidi. Kwa hiyo mabomba ya maji yanawekwa chini ya ardhi kwenye kimo ambako kwa kawaida jalidi haifiki. Lakini kama majirabaridi ni kali sana hata hivyo maji yanaweza kuganda ndani ya mabomba na kupasua bomba. Katika mazingira penye jalidi kunatokea pia uharibifu wa barabara kama maji ya mvua yameingia katika tako la barabara au katika mapengo madogo kwenye lami na kuganda baadaye; maana maji yaliyoganda hupabnuka kidogo na hivyo kupasua lami.
 
Katika mazingira baridi sana kama [[aktiki]] au [[antaktiki]] jalidi unaingia katika udongo hadi kimo cha mita kadhaa. Katika mazingira haya majirajoto ni fupi mno hivyo kuna sehemu za juu za ardhi pekee inayopoa lakini chini yake bado kuna [[jalidi ya kudumu]] (ing. ''permafrost''). Hii inazuia uoto wa miti na kutokea kwa [[tundra]] kwa mfano katika maeneo mapana ya [[Urusi]] wa Kaskazini na [[Alaska]].
 
{{mbegu-sayansi}}