Nairobi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 72:
Kitangulizi cha Nairobi kilikuwa kituo kidogo kilichoanzishwa 1896 kando la mto Nairobi na wakala Mwingereza wa reli kwa kusudi la kuajiri wafanyakazi wazalendo kwa ujenzi wa reli. Mwaka uliofuata 1897 wakaguzi walioandaa njia ya reli walipiga kambi karibu naye. <ref>Christine Stephanie Nicholls, Red Strangers, uk. 37 f.</ref>.
=== Mji mkuu wa koloni===
Njia ya reli ilifika kwenye kambi tarehe [[30 Mei]] [[1899]]. Sasa idadi ya wafanyakazi -hasa Wahindi- iliongezeka sana na kambi lilikuwa kubwa ya ma[[hema]] na [[ghala]] za vifaa vya ujenzi. Mwezi wa Juni mizigo ya mabati ilifika kutoka Mombasa -tayari kwa reli- na majengo ya kudumu yalianza kutengenezwa katika mazingira ya eneo la [[Kituo cha Reli Nairobi|kituo cha reli cha leo]]. Mwezi wa Agosti kamishna Mwingereza wa jimbo la Ukamba<ref>Ukamba ilikuwa moja kati ya majimbo 4 ya [[Afrika ya Mashariki ya Kiingereza]] (iliyokuwa koloni ya Kenya tangu 1920) na makao makuu yalikuwepo Machakos</ref> aliamuliwa kuhamisha makao makuu yake Nairobi kutoka [[Machakos]] akajenga boma lake kwenye eneo la Moi Avenue mbali na reli jinsi inavyoonekana hadi leo kwenye majengo ya polisi ya kihistoria yanayotazama [[Bustani ya Jivanji]]<ref>Kituo cha polisi (Nairobi Central Police Station) iko mahali pa boma lile la kwanza</ref>. Barabara kuu ya kwanza ilikuwa Station Road, ikaitwa baadaye Government road, leo hii ni Moi Avenue. Mtaa wa Tom Mboya wa leo ikaitwa Victoria Street ikawa mahali pa maduka na hoteli za kwanza zilizoendeshwa na Wazungu na baadaye pia na Wahindi kadhaa. Soko la Wahindi maskini likuwa kando. Kwenye sehemu kati ya mitaa ya Haile Selassie na harambee kulikuwa na makazi ya kwanza ya wafanyakazi. Mwaka uleule wa 1899 ofisi kuu ya reli ikapelekwa hapa kutoka Mombasa kwa shabaha ya kurahisisha mawasiliano.
 
Barabara kuu ya kwanza ilikuwa "Station Road" <ref>ikaitwa baadaye Government Road, leo hii ni Moi Avenue</ref> kandokando ya Mtaa wa Tom Mboya wa leo iliyoitwa Victoria Street ikawa mahali pa maduka na hoteli za kwanza zilizoendeshwa na Wazungu na baadaye pia na Wahindi kadhaa. Soko la Wahindi maskini likuwa kando. Kwenye sehemu kati ya mitaa ya Haile Selassie na Harambee kulikuwa na makazi ya kwanza ya wafanyakazi. Mwaka uleule wa 1899 ofisi kuu ya reli ikapelekwa hapa kutoka Mombasa kwa shabaha ya kurahisisha mawasiliano.
 
Pale mwanzoni kulikuwa na wasiwasi kuhusu chaguo la mahali; baada ya mvua kali sehemu ya hema na vibanda ilipatikana katikati ya ziwa la matope. Magonjwa yalisambaa na baada ya epidemia ya tauni soko la wahindi ilichomwa na kuhamishwa sehemu nyingine. Majaribio ya kukausha kinamasi yaliendelea kwa miaka kadhaa hadi kufaulu. Kutokana na usumbufu wa matope maafisa wa ngazi ya juu walijenga nyumba zao kwenye kilima cha karibu kilichojulikana kama Nairobi Hill.
Line 78 ⟶ 81:
Mwaka 1905 Waingereza walihamisha [[ofisi kuu]] ya [[serikali]] yao ya [[ukoloni|kikoloni]] kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ikawa hivyo [[makao makuu]] ya [[Afrika ya Mashariki ya Kiingereza]] (''British East Africa'', baadaye ''Kenya Colony'').
 
Uchumi wa mji ulitegemea pale mwanzoni hasahasa mahitaji ya utawala wa serikali na reli na utalii; matajiri wengi kutoka pande zote za dunia walikuja hapa kwa kusudi la kuwinda wananyama wakubwa <ref>Kama maarufu "Big Five" yaani tembo, simba, nyati, kifaru na chui</ref> wakivutwa na uwingi wa wanyama kwenye nyada za juu na usafiri rahisi kwa reli. Baadaye ardhi ilipewa kwa walowezi wazungu na kilimo cha kibiashara kilianza kuchangia.
 
Kiasili Nairobi ilikuwa imepangwa kwa ajili ya Wazungu wa reli na serikali pamoja na Wahindi; Waafrika hawakupewa makazi isipokuwa mabweni ya wanfanyakazi wa reli na vibanda vya wafanyakazi wasaidizi kandokando ya nyumba za mabwana wao.
 
Lakini Waingereza walikuwa waliajiri askari kutoka Sudan na Somalia katika jeshi na polisi, na hao walifuatwa na wafanyabiashara kutoka kwao. Wapagazi na askari kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki walifika Nairobi kikazi na wengine waliamua kubaki hapa. Mitaa ya vibanda iliota haraka nje ya mji mwenyewe, mingine ilibomolewa haraka, mingine iliweza kubaki. Mnamo 1921 kulikuwa na Waafrika 12,000 waliokaa katika mitaa ya Waafrika iliyoitwa Mombasa, Masikini, Kaburini, Kariokor, Kibera, Pumwani na Pangani.
 
=== Tangu uhuru===
Mwaka 1963 ikawa mji mkuu wa [[nchi huru]] ya Kenya ikaendelea kukua haraka.