Nairobi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 68:
 
=== Chanzo kwenye kambi la reli===
Nairobi ilianzishwa na [[Waingereza]] mwaka [[1899]] kama kambi ya kujenga [[Reli ya Uganda]]. [[Njia ya reli]] ilikuwa imefika kutoka Mombasa ikaonekana ya kwamba kuanzia hapa kasi ya [[ujenzi]] itachelewa kutokana na ugumo na eneo la Bonde la Ufa na mitelemko yake mikali. Mahali palikuwa karibu katikati ya [[Mombasa]] na [[Kampala]], palikuwa na [[maji]] pakaonekana panafaa kwa kituo njiani. Hasahasa ilionekana [[tabianchi]] ya [[nyanda za juu]] ilifaa [[Afya|kiafya]] kwa Waingereza walioteswa na [[joto]] la [[pwani]] na kwenye [[nyanda za chini]].
 
Kitangulizi cha Nairobi kilikuwa kituo kidogo kilichoanzishwa mwaka [[1896]] kando laya [[mto Nairobi]] na wakala Mwingereza wa reli kwa kusudi la kuajiri [[wafanyakazi]] wazalendo kwa ujenzi wa reli. Mwaka uliofuata [[1897]] wakaguzi walioandaa njia ya reli walipiga kambi karibu naye. <ref>Christine Stephanie Nicholls, Red Strangers, uk. 37 f.</ref>.
=== Mji mkuu wa koloni===
Njia ya reli ilifika kwenye kambi tarehe [[30 Mei]] [[1899]]. SasaHapo idadi ya wafanyakazi - hasa [[Wahindi]] - iliongezeka sana na kambi lilikuwa kubwa ya ma[[hema]] na [[ghala]] za vifaa vya ujenzi. Mwezi wa Juni mizigo ya [[mabati]] ilifika kutoka Mombasa - tayari kwa reli - na majengo ya kudumu yalianza kutengenezwa katika mazingira ya eneo la [[Kituo cha Reli Nairobi|kituo cha reli cha leo]]. Mwezi wa Agosti [[kamishna]] Mwingereza wa jimbo la [[Ukamba]]<ref>Ukamba ilikuwa moja kati ya majimbo 4 ya [[Afrika ya Mashariki ya Kiingereza]] (iliyokuwa koloni yala Kenya tangu mwaka 1920) na makao makuu yalikuwepo Machakos</ref> aliamuliwa kuhamisha makao makuu yake Nairobi kutoka [[Machakos]] akajenga [[boma]] lake kwenye eneo la Moi Avenue, mbali na reli jinsi inavyoonekana hadi leo kwenye majengo ya [[polisi]] ya kihistoria yanayotazama [[Bustani ya Jivanji]]<ref>Kituo cha polisi (Nairobi Central Police Station) iko mahali pa boma lile la kwanza</ref>.
 
[[Barabara]] kuu ya kwanza ilikuwa "Station Road" <ref>ikaitwa baadaye Government Road, leo hii ni Moi Avenue</ref> kandokando ya Mtaa wa Tom Mboya wa leo iliyoitwa Victoria Street ikawa mahali pa [[duka|maduka]] na [[hoteli]] za kwanza zilizoendeshwa na [[Wazungu]] na baadaye pia na Wahindi kadhaa. Soko la Wahindi maskini likuwa kando. Kwenye sehemu kati ya mitaa ya [[Haile Selassie]] na Harambee kulikuwa na makazi ya kwanza ya wafanyakazi. Mwaka uleule wa 1899 ofisi kuu ya reli ikapelekwa hapahuko kutoka Mombasa kwa shabaha ya kurahisisha mawasiliano.
 
Pale mwanzoni kulikuwa na wasiwasi kuhusu chaguo la mahali; baada ya [[mvua]] kali sehemu ya hemamahema na vibanda ilipatikanavilipatikana katikati ya ziwa la matope. [[Magonjwa]] yalisambaa na baada ya [[epidemia]] ya [[tauni]] soko la wahindiWahindi ilichomwaLilichomwa na kuhamishwa sehemu nyingine. Majaribio ya kukausha kinamasi yaliendelea kwa miaka kadhaa hadi kufaulu. Kutokana na usumbufu wa matope maafisa wa ngazi ya juu walijenga nyumba zao kwenye [[kilima]] cha karibu kilichojulikana kama Nairobi Hill.
 
Mwaka 1905 Waingereza walihamisha [[ofisi kuu]] ya [[serikali]] yao ya [[ukoloni|kikoloni]] kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ikawa hivyo [[makao makuu]] ya [[Afrika ya Mashariki ya Kiingereza]] (''British East Africa'', baadaye ''Kenya Colony'').
 
[[Uchumi]] wa mji ulitegemea pale mwanzoni hasahasa mahitaji ya utawala wa serikali na reli na [[utalii]]; [[matajiri]] wengi kutoka pande zote za dunia walikuja hapawaliFIka kwa kusudi la kuwinda wananyama[[wanyama]] wakubwa <ref>Kama wale maarufu "Big Five" yaani [[tembo]], [[simba]], [[nyati]], [[kifaru]] na [[chui]]</ref> wakivutwa na uwingiwingi wa wanyama kwenye nyanda za juu na usafiri rahisi kwa reli. Baadaye ardhi katika mazingira ya mji ilipewailitolewa kwa [[walowezi]] wazunguWazungu na [[kilimo cha kibiasharabiashara]] kilianza kuchangia.
 
Kiasili Nairobi ilikuwa imepangwa kwa ajili ya Wazungu wa reli na serikali pamoja na Wahindi; Waafrika hawakupewa makazi isipokuwa [[Bweni|mabweni]] ya wanfanyakazi wa reli na vibanda vya wafanyakazi wasaidizi kandokando ya nyumba za mabwana wao.
 
Lakini Waingereza walikuwa waliajiri [[askari]] kutoka [[Sudan]] na [[Somalia]] katika [[jeshi]] na polisi, na hao walifuatwa na wafanyabiashara kutoka kwao. [[Wapagazi]] na askari kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki walifika Nairobi kikazi na wengine waliamua kubaki hapa. Mitaa ya vibanda iliota haraka nje ya mji mwenyewewenyewe, mingine ilibomolewa haraka, mingine iliweza kubaki. Mnamo [[1921]] kulikuwa na Waafrika 12,000 waliokaa katika mitaa ya Waafrika iliyoitwa Mombasa, Masikini, Kaburini, Kariokor, Kibera, Pumwani na Pangani.
 
=== Tangu uhuru===