Tofauti kati ya marekesbisho "Majadiliano ya mtumiaji:Baba Tabita"

::Asante lakini sidhani ni hii. Naona Mwandishi alikuwa na neno la kiingereza "Cave Art" , "Cave Paintings" akilini mwake. Lakini si kawaida Afrika mahali pengi si hasa mapango (jinsi ilivyo Ulaya penye majirabaridi kali) lakini penye kuta za mwamba penye labda kishubaka au chini ya sehemu inayotokeza kidogo. au jinsi nilivyoona hapa Uajemi ukutani moja kwa moja bila kitu cha juu. Nikitaka kuandika juu ya jumla "Michoro ya mapangoni" ni sehemu tu. Naelekea "Sanaa ya miambani", nasubiri Mkenya kama atajibu, huko kuna NGO ya kuhifadhi african rock art. '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 17:04, 28 Aprili 2016 (UTC)
:::Haya, fanya unavyoona vema. Hata hivyo, kila lugha hubadilisha maana mara kwa mara. Na ingawa michoro = 'paintings' au 'drawings', na mapango = 'caves', maana ya michoro ya mapango siyo "cave paintings" tu. Kule Kondoa vilevile, michoro imechorwa siyo ndani ya mapango tu. Hata maafisa ya Ofisi ya Kale hutumia istilahi ya michoro ya mapango, tena siyo kwa mdomo tu lakini hata kimaandishi. Wasalaam, --'''[[Mtumiaji:Baba Tabita|Baba Tabita]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Baba Tabita#top|majadiliano]])''' 19:29, 28 Aprili 2016 (UTC)
::: Tena ukilinganisha sanaa na michoro, utagundua kwamba neno la michoro hutumiwa mara nyingi zaidi kuliko neno la sanaa, k.m. "sanaa ya miambani" iko mara saba tu mtandaoni kulingana na mara 560 kwa "michoro ya miambani". Naomba tuangalie matumizi ya maneno yanavyotumiwa na watu wengi. Asanteni. --'''[[Mtumiaji:Baba Tabita|Baba Tabita]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Baba Tabita#top|majadiliano]])''' 19:36, 28 Aprili 2016 (UTC)
62,394

edits