Sayari : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 6:
 
==Ufafanuzi wa sayari==
Zamani kulikuwa na sayari 5 tu zilizionekana angani kwa macho matupu kama nyota zinazobadilisha mahali<ref>Hizi ni Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohali. Pale mwanzoni kabla ya uchunguzi wa [[Kopernikus]] haikueleweka ya kwamba Dunia ni sayari sawa na nyingine. </ref>. Tangu kupatikana kwa mitambo kama [[darubini]] katika miaka 400 iliyopita idadi ya magimba angani yenye miendo ya pekee imeongezeka sana lakini ilionekana pia kuna tofauti kubwa sana kati ya magimba haya.
 
Hivyo wataalamu wa [[Umoja wa kimataifa wa astronomia]] (IAU) walikubaliana mwaka [[2006]] kuhusu ufafanuzi wa sayari. Gimba la angani linahesabiwa kuwa sayari kama linatimiza masharti matatu:<ref>[http://www.iau.org/news/pressreleases/detail/iau0603 Azimio 5A ya IAU ya 2006] "The IAU members gathered at the 2006 General Assembly agreed that a "planet" is defined as a celestial body that (a) is in orbit around the Sun, (b) has sufficient mass for its self-gravity to overcome rigid body forces so that it assumes a hydrostatic equilibrium (nearly round) shape, and (c) has cleared the neighbourhood around its orbit." Tangazo kwenye Tovuti ya IAU, IAU 2006 General Assembly: Result of the IAU Resolution votes, iliangaliwa Mei 2016 </ref>