Hakimu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Hakimu''' ni mtu anayetawala kesi mahakamani akiwa peke yake au akiwa kama sehemu ya jopo la majaji. Mamlaka, kazi njia ya uteuzi, nidhamu n...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:08, 22 Mei 2016

Hakimu ni mtu anayetawala kesi mahakamani akiwa peke yake au akiwa kama sehemu ya jopo la majaji. Mamlaka, kazi njia ya uteuzi, nidhamu na mafunzo ya mahakimu yanatofautiana katika mahakama mbalimbali.

Hakimu anatakiwa kuendesha kesi bila kuonyesha upendeleo na katika mahakama ya wazi. Hakimu anasikiliza mashahidi na ushahidi uliowasilishwa na mawakili wa kesi, kisha kutathmini ukweli na hoja za pande mbili tofauti, na kisha anatoa uamuzi juu ya suala hilo kulingana na tafsir yake ya sheria na hukumu yake binafsi.

Katika baadhi ya mahakama, mamlaka ya hakimu inaweza kuwa sawasawa na ya jaji. Katika mifumo ya uchunguzi wa tuhuma hakimu anaweza pia kuwa hakimu mpelelezi.