Difference between revisions of "Wadudu"

4 bytes removed ,  3 years ago
m
no edit summary
m
'''Wadudu''' wa kweli (tazama [[mdudu]]) ni kundi la [[arithropodi]] wadogo kiasi ambalo lina [[spishi]] nyingi [[dunia]]ni. [[biolojia|Kibiolojia]] wako katika [[ngeli]] ya [[Insecta]].
 
Wadudu wanashirikiana kuwa na [[muundo]] wa [[kiwiliwili]] chenye pande tatu za [[kichwa]] mbele, [[kidari]] katikati na [[fumbatio]] nyuma, halafu [[jozi]] tatu za [[miguu]] na kwa kawaida jozi mbili za [[mabawa]]. Kwa nje kiwiliwili kinafunikwa kwa [[khitini]] yenye kazi ya [[kiunzi nje]].
 
Hadi sasa [[wataalamu]] waliainisha zaidi ya spishi [[milioni]] 1 za wadudu na [[kadirio|makadirio]] ni kwamba kuna spishi nyingi zaidi, labda hadi milioni 30.