Tegu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa mpya
 
dNo edit summary
Mstari 36:
** [[Trypanorhyncha]]
}}
'''Mategu''' ni aina za [[mnyoo|minyoo]] yaliyo bapa ([[myoomnyoo-bapa|minyoo-bapa]]) katika [[oda]] [[Cestoda]] na [[faila]] [[Platyhelminthes]]. Mategu waliokoma huishi kama [[kidusia|vidusia]] katika [[mfumo wa mmeng'enyo wa chakula]] wa [[vertebrata]] ambapo hufyunda virutubishi katika giligili ya [[utumbo]]. [[Lava]] wa takriban [[spishi]] zote hukua katika spishi nyingine ya mwenyeji kuliko yule wa wazazi na mara nyingi katika [[arithropodi]]. Wenyeji wakubwa wana spishi kubwa za mategu, k.m. ''Polygonoporus giganticus'' wa [[nyangumi]] ana urefu wa m 30, na wenyeji wadogo wana mategu wadogo, k.m. ''Vampirolepis murini'' wa [[kirukanjia (mamalia)|virukanjia]] ana urefu wa mm 8-15. Tegu anayedusia [[mwanadamu]] mara nyingi, ''Taenia saginata'' ([[Tegu wa Ng'ombe]]), ana urefu wa 20 m.
 
[[Kichwa]] cha tegu huitwa [[skoleksi]] ([[w:scolex|scolex]]) na kina kulabu na/au [[ogani]] za mfyonzo ili kujishikiza kwa ukuta wa utumbo. [[Mwili]] una [[pingili]] nyingi zinazozaliwa mfululizo mwishoni kwa skoleksi. Kila pingili ina ogani za jinsi na zile za mwisho ambazo zina [[yai|mayai]] yaliyoiva, zinaachwa na kutolewa kwa mwili pamoja na mavi. Kama mayai yakiliwa na mwenyeji wa kati lava zinatoa mayai na kukua. Baada ya muda fulani wanaingia kwa [[musuli|misuli]] na kuunda uvimbe ([[w:cyst|cyst]]). Mwenyeji wa kati akiliwa na [[mbuai]] lava wanakomaa katika utumbo.