Tofauti kati ya marekesbisho "Tanganyika African National Union"

+kuboresha makala
(+picha na maelezo yake)
(+kuboresha makala)
 
TANU ilishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni ikawa chama cha kuongoza Tanganyika hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961. [[Katiba]] ya Taifa ya mwaka 1962 ilifanya TANU kuwa chama cha pekee nchini ikifuata mfano wa [[nchi za kijamaa]] zenye muundo wa [[siasa ya chama kimoja]].
==Mtiririko wa upatikanaji uhuru==
Mtiririko wa kupigania uhuru wa Tanganyika na mchango wa Mwalimu katika kupigania uhuru:
 
1929: TAA yaundwa ikiwa na wajumbe wafuatao:
 
1. Kleist Sykes
2. Mzee bin Sudi
3. Ibrahim Hamis
4. Zibe Kidasi
5. Ali Said Mpima
6. Suleiman Majisu
7. Raikes Kusi
8. Rawson Watts
9. Cecil Matola
 
1950: TAA yawasiliana na KAU; Abdulwahid alikwenda [[Nairobi]] kukutana na [[Jomo Kenyatta]] ili kujenga mawasiliano na chama cha [[Kenya African Union]] (KAU).
 
1951: Kuundwa kwa tawi la siasa la [[TAA]]; likiwa na wajumbe wafuatao:
 
1. [[Abdulwahid Sykes]] (Katibu)
2. [[Sheikh Hassan bin Amir]]
3. [[Hamza Kibwana Mwapachu]]
4. [[Said Chaurembo]]
5. Dk. Kyaruzi.
6. [[John Rupia]]
7. [[Stephen Mhando]]
 
1951: Kenyatta akutana tena na viongozi wa TAA. Safari hii mkutano huo ulifanyika [[Arusha]]. Wajumbe wa TAA walikuwa Abdulwahid Kleist Sykes, [[Dossa Aziz]] na [[Stephen Mhando]].
 
1952: Abdulwahid alichaguliwa kuwa Rais wa TAA.
 
1952: Mwalimu Nyerere atambulishwa kwa Abdulwahid na Bwana Kasela Bantu. Baada ya utambulisho huo ikawa kila Jumamosi Mwalimu Nyerere akawa anakutana na akina Dossa Azizi, Bw. [[Ally Sykes]], Abdulwahid Sykes, Dustan Omar na Mhando kujadili mustakbali wa nchi ya Tanganyika.
 
Mikutano hiyo ama ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Dossa Azizi mtaa wa Congo au mtaa wa Stanley nyumbani kwa Abdulwahid.
 
Alikuwa ni Dossa Azizi ambaye mara nyingi alikuwa akimrudisha Mwalimu Nyerere kwa gari lake Pugu (St. Francis College) baada ya mkutano.
 
1953: Mwalimu achaguliwa kuwa Rais wa TAA. Wazee waliompa nguvu ya kisiasa Mwalimu mara baada ya kuingia katika TAA/TANU.
 
[[Sheikh Hassan bin Amir]], [[Sheikh Suleiman Takadir]], Mzee [[Mohammed Jumbe Tambaza]], [[Mshume Kiyate]] na [[Mwinjuma Mwinyikambi]]. Wengine walikuwa Rajab Diwani, [[Makisi Mbwana]], Sheikh Haidar Mwinyimvua na [[Idd Faiz Mafongo]]. Aidha walikuwepo Idd Tosiri, [[Sheikh Mohamed Ramia]] na Mashado Ramadhani Plantan.
 
Oktoba 10, 1953 Mwalimu Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia walikutana kujadili namna ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa.
 
1954: TANU yaanzishwa. Wajumbe wa mkutano uliojadili kuibadili katiba ya TAA kuwa TANU walikuwa Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere, [[Tewa Said Tewa]], Dossa Aziz, Ally Sykes, Kasela Bantu, , Abubakar Ilanga na [[Saadan Abdu Kandoro]]. Wengine walikuwa S.M. Kitwana, C.O. Milinga, Patrick Kunambi, Gerimano Pacha, Japhet Kirilo na L.M. Makaranga. Walikuwa pia Joseph Kimalando na John Rupia.
 
Mkutano wa kuizindua rasmi TANU ulihudhuriwa na wajumbe wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na Mshume Kiyate. Wengine walikuwa Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan na Marsha Bilali. Walikuwepo pia Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengine.
 
Julius Nyerere alipewa kadi ya TANU Na. 1, kadi Na. 2 ikaenda kwa Ally Sykes na Abdulwahid akachukua kadi ya TANU Na. 3, Dossa Azizi alichukua kadi Na. 4, kadi Na. 5 ikaenda kwa Phombeah. Dome Okochi alipata kadi Na. 6, John Rupia Na. 7, Bibi [[Titi Mohamed]] kadi Na. 16 na Idd Tosiri kadi Na. 25.
 
[[Category:Siasa ya Tanzania|TANU]]