Bibi Titi Mohammed : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
neno kuntu na picha
Mstari 1:
[[Picha:Titi Mohamed.JPG|thumb|'''Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la Magomeni Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar wa tano Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi wa saba Mama Tindwa waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na wa tatu ni Bi. Titi Mohamed na pembeni ni mwanae.''']]
'''Bibi Titi Mohammed''' ([[1926]] - [[5 Novemba]] [[2000]]) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza mzalendo kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini [[Tanzania]]. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa [[Tanganyika]].
 
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais [[Julius Nyerere]].