Tofauti kati ya marekesbisho "Migoli"

10 bytes removed ,  miaka 6 iliyopita
d
wa wa --> wa; new lines; double spaces using AWB
d (Bot: Replacements: fix URL prefix)
d (wa wa --> wa; new lines; double spaces using AWB)
'''Migoli''' ni [[mji mdogo]] kwenye [[Wilaya ya Iringa Vijijini]] katika [[Mkoa wa Iringa]], [[Tanzania]]. Iko mita 700 juu ya usawa wa bahari.
 
Unapatikana kando ya [[Bwawa la Mtera]] ambako wakazi wengi hutegemeza maisha yao katika [[uvuvi]].
 
Eneo hili lina [[rutuba]] lakini [[mvua]] ni chache (kwa kawaida haifikii mm. 300 kwa mwaka), hivyo wakazi hawajishughulishi sana na [[kilimo]], hivyo wananunua [[nafaka]] kutoka sehemu ambazo zinalimwa kwa wingi, kama vile [[Ismani]] tarafani na [[Mtamba]] [[mkoa wa Dodoma]].
Kumbe ni eneo maarufu kwa [[ufugaji]], hasa wa [[ng'ombe]] na [[mbuzi]], wanaostawi katika [[mbuga]] isiyo na [[malale]].
 
Eneo hili, ambapo inapita [[barabara]] kuu ya [[Afrika]] kutoka [[Misri]] hadi [[Afrika Kusini]] (ingawa sehemu hii kati ya [[Dodoma]] na [[Iringa]] haimalizika kutiwa lami), ni endelevu hasa ukilinganishwa na vijiji vingine vya nchi ya Tanzania, kwa kuwa una huduma nyingi za jamii ambazo zimetokana na juhudi za [[serikali]] na wananchi wenyewe.
 
Wafadhili wa miradi mbalimbali ni kama vile [[parokia]] [[Kanisa Katoliki|katoliki]] ya Migoli na makampuni ya mawasiliano kama vile Zain, Tigo, Vodacom na Zantel.
 
Kijiji asili kilikua sana baada ya [[serikali]] kuanza kujenga bwawa la Mtera na kulazimisha watu walioishi bondeni na pembezoni mwa mkondo wa [[mto Ruaha]] wasogee ikiwa ni [[miaka ya 1980]]. Wazee wa kwanza walioshi katika mitaa miwili ya Migoli na Makonge walikuwa Maulidi Ndilwa, Nyakunga, Simili Magomba, [[Paulo Magomba]], Madekedeke, Kinyaga pamoja na [[familia]] zao.
 
Tangu kuanzishwa kwa Bwawa la Mtera na kijiji cha Migoli, shughuli ya uvuvi ilikikuza sana kijiji cha Migoli ambacho kimekuwa mahali pa [[biashara]] yaani watu kutoka makambini (makazi yasiyo rasmi ya uvuvi) walikuwa wakiuzia [[samaki]] kwenye kijiji cha Migoli.
 
Hata hivyo wafanyabiashara wa samaki wamekitumia kijiji cha Migoli kuwa sehemu yao ya kufikia kabla ya kwenda kwenye makambi. Makambi yanayokitegemea kijiji cha Migoli ni Nyegere, Mabati, Maperamengi, Mandela, Kilambakitali, Changalawe na mengine mengi.
Hatimaye kijiji kimemegwa na kuzaa kijiji kipya cha [[Mtera]] upande wa kaskazini.
 
WakatiKwa wamujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Migoli ilikuwa na wakazi wapatao 10,937 waishio humo. <ref>[http://www.wavuti.weebly.com/uploads/3/0/7/6/3076464/census20general20report20-202920march202013_combined_final20for20printing1.pdf Sensa ya 2012, Iringa Region- Iringa District Council]</ref>
Siku hizi [[barabara]] inayopita kijijini ikiunganisha [[Iringa]] na [[Dodoma]], hivyo pia [[Cape Town]] na [[Kairo]], imetiwa [[lami]].
 
==Marejeo==
{{marejeo}}
{{marejeo}} {{Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini}} [[Jamii:Wilaya ya Iringa Vijijini]] [[Jamii:Mkoa wa Iringa]] {{mbegu-jio-iringa}}
{{Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini}}
 
{{mbegu-jio-iringa}}
 
[[Jamii:Wilaya ya Iringa Vijijini]]
[[Jamii:Mkoa wa Iringa]]
62,394

edits