Tofauti kati ya marekesbisho "Elimu"

12 bytes added ,  miaka 4 iliyopita
d
no edit summary
d
'''Elimu''' kwa [[maana]] pana ni [[tendo]] au uzoefu wenye [[athari]] ya kujenga [[akili]], [[tabia]] ama [[uwezo]] wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika [[dhana]] ya ki[[ufundi]], elimu ni [[njia]] ambayo hutumiwa ma[[kusudi]] na jamii kupitisha [[maarifa]], [[ujuzi]] na [[maadili]] kutoka kwa [[kizazi]] kimoja hadi kingine.
 
[[Walimu]] katika [[taasisi]] za elimu huratibisha elimu ya [[wanafunzi]] wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, [[hesabu]] au hisabati, [[sayansi]] na [[historia]]. [[Mbinu]] hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea [[somo]] la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na ma[[profesa]] katika taasisi za masomo ya juu.
 
Kuna [[elimu maalumu]] kwa wale wanaohitaji ujuzi wa kitaaluma, kama vile wale wanaohitaji kuwa [[rubani|marubani]]. Juu ya hayo, kuna nafasi nyingi za elimu katika viwango vingine visivyo rasmi kama vile [[Makumbusho|majumba ya ukumbusho]], [[maktaba]] pamoja na [[mtandao]] na [[tajriba]] za [[maisha]].