Foxy Brown : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Infobox person | jina = Foxy Brown | picha = Foxy-brown.jpg | alt = | maelezo = Brown at the 2007 Olympus...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 04:53, 19 Julai 2016

Inga DeCarlo Fung Marchand (amezaliwa tar. 6 Septemba, 1978),[2] anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Foxy Brown, ni rapa, , mwanamitindo, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anajulikana sana kwa kazi zake za kujitegemea,, vilevile kwa kazi zake kushirikiana na wasanii mbalimbali hasa kwa uhusiano wa muda mfupi na kundi zima la muziki wa hip hop - babu-kubwa The Firm. Amekulia mjini Brooklyn, New York, baba yake mzazi mzee Keith Stahler aliitelekeza familia yake akiwa mdogo mno ili kwenda kuendeleza kazi zake katika studio ya ERAC records. Albamu zake ni pamoja na Ill Na Na mnamo 1996, ikafuatiwa na Chyna Doll mnamo 1999, na Broken Silence mnamo 2001. Vilevile amerap katika albamu ya kundi lake shirikishi mnamo 1997 ya the Firm, The Album, albamu pekee iliyopata kutolewa na kundi hilo hadi sasa. Katika kazi zake, Brown anarekodi mbaya mno ya kutiwa mbaroni na kutumikia kifungo mara kadhaa.

Foxy Brown
Faili:Foxy-brown.jpg
Brown at the 2007 Olympus Fashion Week
AmezaliwaInga DeCarlo Fung Marchand[1]
6 Septemba 1978 (1978-09-06) (umri 45)[nb 1]
Majina mengine
  • Brooklyn's Don Diva
  • Chyna Doll
  • Fox Boogie Brown
  • Ill Na Na
Kazi yake
  • Rapper
  • mtunzi wa nyimbo
  • mwanamitindo
  • mwigizaji
Miaka ya kazi1994–hadi sasa
Foxy Brown

Baada ya 2001, aliendelea kurekodi mistari kwa ajili yake mwenyewe na wasanii wengine lakini hajatoa albamu yoyote ile; ametoka katika studio ya Def Jam mnamo 2003, hivyo basi inapeleka kughairishwa kwa kutolewa kwa albamu yake ya pili ya Ill Na Na 2. Hata hivyo, alirudi katika studio hiyo mnamo Januari 2005 baada ya Jay-Z kuwa Rais na CEO wa Def Jam na kuingia mkataba upya na kuanza kazi ya albamu yake mpya iliyoitwa Black Roses. Mnamo Desemba 2005, akaanza kusumbuliwa na matatizo ya kutosikia, ambapo ilipelekea kusimama kwa kazi zake hadi kiangazi kilichofuata, miazi michache baada ya kufanyiwa upasuaji. Albamu yake ya nne, ambayo awali ikuwa kandamseto, ilitolewa mnamo mwezi wa Mei 2008 ikiwa fuatiwa na machelewesho kedede yaliyotokana na kifungo cha jela kilichosababishwa na ukorofi wake Brown.

Kazi za muziki

Diskografia

Filmografia

Mwaka Jina Uhusika
1998 Woo Fiancée
2004 Fade to Black Fox Brown

Marejeo

  1. Brown, Scott. "Lil' Brown & Co.", 2001-03-09. Retrieved on 2008-02-29. 
  2. 2.0 2.1 "Foxy Brown Busted". The Smoking Gun. February 16, 2007. Iliwekwa mnamo December 31, 2009.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Contrite
  4. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named allmusic
  5. "I Don't Need Nobody" on YouTube

Viungo vya Nje

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Foxy Brown

Kigezo:Authority control
Hitilafu ya kutaja: <ref> tags exist for a group named "nb", but no corresponding <references group="nb"/> tag was found