Klabu za Kiswahili : Tofauti kati ya masahihisho
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Yafuatayo ni baadhi ya malengo ya kuanzinshwa kwa klabu mbalimbali za Lugha ya Kiswahili katika shule mbalimbali za sekondari nchini Tanzania. <nowiki>*</nowik...' |
(Hakuna tofauti)
|
Pitio la 13:06, 11 Septemba 2016
Yafuatayo ni baadhi ya malengo ya kuanzinshwa kwa klabu mbalimbali za Lugha ya Kiswahili katika shule mbalimbali za sekondari nchini Tanzania.
*1.Kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.
*2.Kudumisha umoja na mshikamano kwa watumiaji wa Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.
*3.Kujifunza zaidi juu ya misamiati mipya ya Lugha ya Kiswahili baina ya watumiaji {Kupitia midahalo na majadiliano}.
*4.Kuibua wataalamu hodari wa kutumia Lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Lugha ya Kiswahili{sarufi ya Kiswahili},yaani katika kimatamshi,kimantiki na kimaana.
*5.Kuandaa wasanifishaji hodari wa Lugha ya Kiswahili au kufanya uwiano sawa wa kimatamshi katika Lugha.
*6.Kuibua vipaji mbalimbali vya sanaa mfano watunzi wa nyimbo{mashairi},ngonjera,hadithi{simulizi za kusisimua} na majigambo.Kwa lengo la kueneza tamaduni za Kiswahili{Mswahili}.
*7.Kuibua waandaaji hodari wa hotuba za Kiswahili ndani na nje ya nchi ya Tanzania kwa uzingatiaji wa kanuni,taratibu na sheria zote za uandaaji wa hotuba.
*8.Kuandaa wamahiri bora wa Lugha ya Kiswahili yaani wanaoweza kutumia Lugha ya Kiswahili katika nyanja kuu nne ambazo ni kusoma,kuandika,kusikiliza na kuzungumza kwa ufasaha.
*9.Kuandaa wakalimani hodari wa Lugha ya Kiswahili ambao watahamasisha wageni wengi kuwa na shauku ya kujifunza Lugha ya Kiswahili.
*10.Kuandaa watunzi bora wa kamusi za Kiswahili sanifu.