Vijana na Kiswahili : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ' Katika taifa lolote vijana ndio chachu ya maendeleo.Tanzania kuna idadi kubwa ya vijana ambao ndio wanaotegemewa zaidi na taifa letu.Lakini jambo la kushanga...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:15, 11 Septemba 2016

  Katika taifa lolote vijana ndio chachu ya maendeleo.Tanzania kuna idadi kubwa ya vijana ambao ndio wanaotegemewa zaidi na taifa letu.Lakini jambo la kushangaza vijana hao ndio hawana uzalendo na lugha yao ya taifa.Hii ni kutokana na kuonekana wazi kuwa lugha ya Kiswahili haipewi kipaumbele ukilinganisha na lugha nyingine hasa lugha za kigeni.
  Hili janga linatokana na vijana kujiona tumestaarabika kwa kupata elimu ya kutoka kwa watu wa magharibi tunayofundishwa kwa lugha za kigeni.Na hivyo kujikuta lugha yetu tunaizarau na ndiyo chanzo cha ukasumba ndani ya nchi yetu.Kwakuwa vijana ndio tunaopata elimu hii,hatuna budi kukaa na  kuchambua yaliyo mema na kuyafanyia kazi na ndio maana tunathubutu kusema 'vijana ndiyo chanzo cha kudumaza Lugha ya Kiswahili' kwa sababu zifuatazo;

1.ELIMU.

  Elimu tunayoipata tunafundishwa kwa kutumia Lugha za kigeni hasa kwa wanafunzi wa    shule za sekondari maana mitaala yao mingi inatumia lugha ya kiingereza na hivyo lugha ya kiswahili kuonekana haina tija.

2.UTAWALA.

  Utawala ndio unahusika na kuaandaa vijana kwa kutoa elimu inayo dumaza lugha ya Kiswahili kwa kutokufanyia mabadiliko ya mitaala ya elimu kwa ngazi za elimu ya sekondari na vyuo maana ndio hutoa vijana wanaokuwa na ukasumba na lugha yao ya kiswahili kwa sababu tofautitofauti wanazojaribu kuzitoa.

3.MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

   hii husababishwa na vijana wengi ambao hujiona kama hawakustaili kuwa na lugha ya kiswahili kutokana na mazoea ya kutumia mambo yaliyotumiwa au yaliyofantwa na yanayofanywa na wageni ambao kwa namna moja ama nyingine wamewaathiri vijana wazawa ambao sasa wanaona ndio msingi wa maisha yao ya kila siku.

4.VIJANA WENGI HUPENDA KUTUMIA MISIMU.

    Misimu mingi itumiwayo na vijana wengi huwa sio sanifu na huwa imechukua maneno mengi kutoka katika lugha za kigeni ambazo hayizina sarufi inayofanana na sarufi ya lugha ya kiswahili. 

5.VYOMBO VYA MAWASILIANO.

    Vyombo vya mawasiliano mfano huruu{simu} vyombo hivi vimeandikwa kwa lugha ya kiingereza ambayo ndio lugha wanayotumia wanafunzi wote wa shule za sekondari na vyuo 

6.VIJANA KUTO KUKUBALI MABADILIKO.

   Vijana walio wengi huwa hawako tayari kupokea mabadiliko mfano:wanapokuwa mahakamani ambako sheria nyingi zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza,huwa hazifanyii mabadiliko yoyote ya lugha yao kwa kuzibadili kwenda katika lugha ya kiswahili.