Rosetta (kipimaanga) : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
+kiungo |
mwisho |
||
Mstari 4:
'''Rosetta''' ni [[chombo cha angani]] cha [[Mamlaka ya Ulaya ya Usafiri wa Anga]]. Kilirushwa [[anga]]ni kutoka kituo cha angani [[Kourou]] mwaka [[2004]] kwa [[roketi]] ya [[Ariane 5]] kwa kusudi la kufikia [[nyotamkia]] ya [[67P/Churyumov–Gerasimenko]].
==Teknolojia==
Ilhali hakuna [[roketi bao]] yenye nguvu ya kufikisha chombo moja kwa moja hadi nyotamkia, Rosetta ilitumia njia ya kuzunguka mara kadhaa [[Dunia]] yetu na [[sayari]] ya [[Mirihi]] kwa kusudi la kuongeza mwendo wake kwa msaada wa [[graviti]] ya sayari hizi.
Rosetta inapata nguvu yake kwa kutumia [[seli]] za [[umemenuru]]. Ilhali [[nuru]] ya jua inapungua sana nje ya njia ya Mirihi, chombo kiliingia katika kipindi kirefu cha [[usingizi]] wa miezi 31 kwa kusudi la kutunza [[nishati]] ya [[beteri]] zake hadi kukaribia lengo lake. Tarehe [[20 Januari]] [[2014]] chombo kiliamka tena wakati wa kukaribia nyotamkia.
==Kufikia nyotamkia==
Mwezi wa Agosti 2014 ilifika ikaanza kuzunguka nyotamkia hiyo. Mwezi wa Novemba 2014 ilirusha lander yake Philae ambayo ilishuka kwenye uso wa nyotamkia tarehe [[11 Novemba]] 2014 ikiwa mara ya kwanza ya chombo kilichotengenezwa na [[binadamu]] kufikia kwenye nyotamkia yoyote.
==Mwisho==
Tarehe 30 Septemba 2016 mnamo saa nane na nusu mchana (saa 13:19 h wakati wa Afrika za Mashariki) shughuli za Rosetta zilifikia mwisho ilhali chombo hiki kiligonga uso wa nyotamkia 67P. Viongozi wa mradi wake waliamua kumaliza kazi kwa njia hii kwa sababu chombo kilifuatana na nyotamkia kwenye njia yake kuelekea ng'ambo ya mzingo wa sayari ya [[Mshtarii]] ambako nuru ya jua haitoshi tena kutosheleza mahitaji ya nishati ya chombo. Hivyo mabaki ya umeme katika beteri yalitumiwa kuwasha injini mara ya mwisho na kukilenga chombo kwenda usoni wa nyotamkia na kutumia safari hii ya mwisho kuchukua tena picha za karibu na kuzituma duniani..
==Viungo vya Nje==
*[http://unawetanzania.org/2014/11/13/mafanikio-yamefikiwa-kutua-juu-ya-kimondo Mafanikio Yamefikiwa: Kutua Juu ya Kimondo; Blogu ya unawetanzania.org kuhusu Rosetta]
|