Papa Nikolasi I : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Superseded by superior version (GlobalReplace v0.6.2)
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Pope Nicholas I.jpg|thumb|right|Mt. Nikolasi I.]]
 
'''Papa Nikolasi I''' au '''Nikolasi Mkuu''' (takriban [[820]] – [[13 Novemba]] [[867]]) alikuwa [[papa]] kuanzia [[24 Aprili]] [[858]] hadi [[kifo]] chake.
 
Alimfuata [[Papa Benedikto III]] akafuatwa na [[Papa Adriano II]].
 
Anakumbukwa kwa kuimarisha [[mamlaka]] wa Papa wa [[Roma]], akichangia ustawi wa [[cheo]] hicho hasa katika [[Ulaya Magharibi]]. Alisisitiza kuwa mamlaka hiyo iko juu ya watawala pia katika masuala ya [[imani]] na [[maadili]].
 
Alikataa kutangaza [[ubatili]] wa [[ndoa]] ya [[mfalme]] [[Lothari II]] wa [[Lotharingia]] na [[mke]] wake, ingawa mfalme aliudai ili kumuoa Waldrada, [[mtaguso]] fulani uliukubali na [[jeshi]] la [[Wafaranki]] lilizingira Roma.
 
Mahusiano na [[Dola la Roma Mashariki]] yaliharibika kwa sababu aliunga mkono [[Patriarki]] [[Ignas wa Konstantinopoli]] aliyekuwa ameondolewa madarakani ili kumpisha [[Fosyo]].
 
Anaheshimiwa na [[Kanisa Katoliki]] kama [[mtakatifu]]. [[Sikukuu]] yake ni tarehe 13 Novemba.