Vitendawili : Tofauti kati ya masahihisho

ajenga ingawa Hana mikono
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Vitendawili''' Vitendawili ni usemi uliofumbwa ambao hutolewa kwa hadhira ili ufumbuliwe,fumbo hilo huwa lina mawazo au mafunzo muhimu kwa hadhira washir...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:08, 8 Oktoba 2016

Vitendawili Vitendawili ni usemi uliofumbwa ambao hutolewa kwa hadhira ili ufumbuliwe,fumbo hilo huwa lina mawazo au mafunzo muhimu kwa hadhira washiriki na kuchemsha au kufikirisha akili zao.

Vitendawili hufikirisha na kuwafanya watu wahusishe na hali halisi maisha na vitu au matukio mbalimbali katika mazingira yao na dunia kwa ujumla.

Mifano ya vitendawili ni 1*Popo mbili zavuka mto(macho). 2*Wazungu wanachungulia dirishani(makamasi). 3*blanketi la babu lina chawa(mbingu).

Vitendawili vina utaratibu maalumu a kuvianza Mfano Mtegaji:Kitendawili? Hadhira:Tega. Mtegaji:Popo mbili zavuka mto? Hadhira:Jua. Mtegaji:Mmekosa!,nipeni mji. Hadhira:Nenda arusha. Mtegaji:Siendi. Hadhira:Nenda Ifakara. Mtegaji:Naenda,jibu lake macho.