Kazi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 16:
 
[[Sheria]] mbalimbali zinaratibu mahusiano kazini, hasa kama kuna [[mwajiri]] na [[mwajiriwa]].
 
==Kazi katika Biblia==
[[Biblia]] inazungumzia maisha halisi ya watu, hivyo haikuweza kuisahau kazi. Toka [[kitabu cha Mwanzo]] inaonyesha heshima ya kufanya kazi kwa kumchora [[Mungu]] akitenda kazi kama binadamu kwa [[siku]] [[sita]], akipumzika ile ya [[saba]].
 
Ndiye aliyewaagiza [[Adamu]] na [[Eva]] wafanye kazi katika [[dunia]] ili kuistawisha.
 
Baada ya [[dhambi ya asili]] waliyoifanya wajibu huo umebaki, ila kama [[adhabu]] sasa unachosha.
 
Pamoja na hayo, [[Yesu]] alikubali kufanya kazi kwa [[mikono]] yake kama [[fundi]] (labda [[seremala]]) kwa sehemu kubwa kabisa ya maisha yake, alipoishi na [[familia]] yake au walau [[mama]] yake [[Kijiji|kijijini]] [[Nazareti]].
 
[[Mtume Paulo]] alipinga kwa nguvu [[uzembe]] wa waliodai kazi haihitajiki tena kwa sababu eti, [[ufalme wa Mungu]] umefika. Alisema, "Asiyetaka kufanya kazi, asile chakula". Mwenyewe, pamoja na kuhubiri [[Injili]] alikuwa akiendelea na kazi yake ya [[Ushonaji|kushona]] [[hema|mahema]] ili kupata mahitaji yake bila kulemea wengine.
 
==Viungo vya nje==
*[http://www.ilo.org/] Tovuti rasmi ya International Labour Organization
 
{{mbegu}}