Kisonono : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 2:
[[Image:Gonococcal lesion on the skin PHIL 2038 lores.jpg|thumb|Dalili ya ugonjwa katika ngozi.]]
[[File:Gonococcal ophthalmia neonatorum.jpg|thumb|Dalili ya mtoto aliyezaliwa na mama mwenye kisonono.<ref>{{cite web|url=http://www.phac-aspc.gc.ca/publicat/clinic-clinique/pdf/s1c16e.pdf|title=Prophylaxis for Gonococcal and Chlamydial Ophthalmia Neonatorum ''in'' the Canadian Guide to Clinical Preventative Health Care|publisher=Public Health Agency of Canada}}</ref>]]
'''Kisonono''' au '''kisalisali''' ni [[maradhi ya zinaa]] ambayo husababishwa na [[bakteria]] zinazofahamika kisayansi kama ''Neisseria gonorrhoeae''. Bakteria hizo hushambulia [[utandotelezi]] unaozunguka [[sehemu za siri]].
 
Ingawa kwa makisio maambukizi 360,000 ya kisonono huripotiwa kila mwaka nchini [[Marekani]], wataalamu wamekisia kuwa watu karibia 650,000 huambukizwa kwa mwaka. Kimataifa yanakadiriwa kuwa kati ya milioni 33 na 106 kwa mwaka. Wagonjwa ni 0.8% ya [[wanawake]] wote na 0.6% ya [[wanaume]] wote.
 
Kama ilivyo [[klamidia]], kisonono nayo huwa haionyeshi [[dalili]]. Kisonono ikiwepo huwa na dalili kama zile za [[klamidia]] ambazo huhusisha mauvimu wakati wa kukojoa na kutokwa kwa [[maji]] yanayonuka au [[usaha]] katika [[uke]] au [[uume]].
 
Kisonono huonekana kwa urahisi kwa wanaume ambao hutoa [[usaha]] kutoka katika [[mfereji wa mkojo]] (''urethra''). Huanza kidogo, lakini huongezeka na huwa mwingi na kusababisha kusikia haja ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa na maumivu.
 
Kisonono ikisambaa na kufikia ''[[tezi kibofu]]'', mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi fulani. Kwa wanawake maambuki hutokea katika [[urethra]], [[uke]] au [[mlango wa uzazi]] (''cervix''). Ingawa mwasho unaotokana na majimaji katika uke unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizi huwa ni chache au hamna kabisa katika hatua za awali.
 
Kisonono isiyotibiwa inaweza kusababisha PID kwa wanawake. [[Watoto]] wanaozaliwa na mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambukizo haya yanaweza kusababisha magonjwa ya [[meno]] kwa wachanga.
 
Uchunguzi wa ugonjwa hufanywa kwa kuchungunza usaha kutoka katika uke au uume au mkojo kwa uwepo wa ''Neisseria gonorrhoeae''.
 
Kisonono iliongezeka kwa kiasi kikubwa [[Marekani]] mnamo [[miaka ya [[1970]] na mwanzoni mwa [[miaka ya [[1980]], hadi kukaribia kufikia kiwango cha [[magonjwa ya mlipuko]] (''epidemic proportions'') kwa [[vijana]] [[balehe|wanaobalehe]] na watu wa [[umri wa kati]].
 
Kisonono hutibiwa kwa [[antibiotiki]] kadhaa, ingawa maambukizi yamekuwa na ukinzani juu ya [[tiba]] ya baadhi ya madawa katika miongo ya nyuma. Moja kati ya mambo magumu katika kupambana na [[kisonono]] ni kutafuta mahusiano yote ya kimapenzi ya nyuma ya aliyeambukizwa ili kuweza kuzuia usambaaji zaidi wa ugonjwa.
 
{{mbegu-tiba}}
 
[[Jamii:Maradhi ya zinaa|Kisonono]]