Burundi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 116:
Mwaka [[1894]] [[Mjerumani]] wa kwanza alipita Burundi aliyekuwa [[Oskar Baumann]]. Wakati ule [[Ujerumani]] uliwahi tayari kuanzisha [[koloni]] ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] lakini Wajerumani walichelewa kufika kaskazini-magharibi mwa maeneo waliyotazama kuwa sehemu yao.
 
Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo [[1896]] wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika [[mji mkuu]] [[Gitega]] ambaye hakuhusika na mambo ya utawala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "[[Urundi]]". Hapa sawa na Rwanda na [[Bukoba]] Wajerumani walitumia [[mbinu]] ya [[eneo lindwa]] ingawa walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni lao.
 
Baada ya [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]] Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa [[Ubelgiji]] kwa niaba ya [[Shirikisho la Mataifa]] kama [[eneo la kudhaminiwa] lililoitwa Ruanda-Urundi. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwachia mtemi [[mamlaka]] kubwa. Waliweka Ruanda-Urundi chini ya serikali ya Kongo ya Kibelgiji.
Mstari 124:
Tangu 1946 Shirikisho la Mataifa lilikwisha na Ubelgiji ilipokea wito wa kutawala Ruanda-Urundi na [[Umoja wa Mataifa]].
[[Picha:BujumburaFromCathedral.jpg|300px|thumbnail|Jiji la Bujumbura]]
 
=== Uhuru ===
Mwaka moja kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi ya [[UM]] na chama mshindi kilikuwa UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi [[Louis Rwagasore]] aliyemwoa [[mwanamke]] wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili. Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na ukabila.