Tanganyika (ziwa) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 26:
 
==Jina==
Jina la ziwa limepokelewa na wapelelezi wazungu wa kwanza kutoka kwa wenyeji wa Ujiji. [[Henry Morton Stanley]] aliyetembelea ziwa mnamo mwaka 1876 aliandika ya kwamba watu wa Ujiji hawakuwa na uhakika kuhusu maana ya jina ila tu ilimaanisha ziwa kubwa<ref>Habari yafuatayaozifuatazo kutoka HM Stanley, [https://archive.org/stream/throughdarkconti1878stan2#page/n31/mode/2up Through the Dark Continent Vol 2, p 16] </ref>. Maana waliita maziwa madogo "Kitanga", na waliita pia "ziwa la Usukuma" yaani Viktoria Nyanza kwa jina hili "Tanganika". Wajiji walimwambia Stanley ya kwamba labda neno "nika" ilitoka kwa aina ya samaki waliyoita vile. Baadaye Stanlea alikumbuka neno "nika" katika lugha nyingine za Kiafrika kwa maana ya "tambarare, eneo kubwa bapa" akahisi ya kwamba waliita ziwa kama "tambarare kubwa iliyotandikwa" <ref>Tanganika, 'the great lake spreading out like a plain', or 'plain-like lake'</ref> .
 
Stanley alishika pia majina ya ziwa kwa makabila mengine- watu wa Marungu walisema "Kimana", wale wa Urungu "Iemba" na Wakawendi "Nsaga" kwa maana "ziwa lenye dhoruba". Alichoshika na watu wa Urungu yaani "Iemba" inalingana na taarifa ya Livingstone aliyekuta jina "Liemba" linaloendelea kutumiwa kwa meli ya [[MV Liemba]] kwenye ziwa.