Mkoa wa Dodoma : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Maandishi yaliyokuwepo yalichukuliwa nafasi na 'the way to anywhere is starting from where you are D !'
d Masahihisho aliyefanya 154.118.225.162 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Kipala
Mstari 1:
[[Picha:Tanzania Dodoma location map.svg|thumb|right|260px|Mahali pa Mkoa wa Dodoma katika [[Tanzania]]]]
the way to anywhere is starting from where you are
[[Picha:Un-tanzania-Kondoa.png|thumb|right|300px|Mkoa wa Dodoma]]
'''Mkoa wa Dodoma''' uko katikati ya Tanzania umepakana na mikoa ya [[Mkoa wa Manyara|Manyara]], [[Mkoa wa Morogoro|Morogoro]], [[Mkoa wa Iringa|Iringa]] na [[Mkoa wa Singida|Singida]]. Sehemu kubwa ya eneo lake ni [[nyanda za juu]] kati ya [[mita]] 830 hadi 2000 juu ya [[UB]].
 
Eneo lote la mkoa lina 41,310 [[km²]]. Kuna [[wilaya]] saba zifuatazo:
 
[[Wilaya ya Bahi]], [[Wilaya ya Chamwino]], [[Wilaya ya Chemba]], [[Wilaya ya Dodoma Mjini]], [[Wilaya ya Kondoa]], [[Wilaya ya Kongwa]], [[Wilaya ya Mpwapwa]]. Wilaya ya awali ya [[Wilaya ya Dodoma Vijijini|Dodoma Vijijini]] imegawiwa kwa wilaya mpya za Chamwino na Bahi.
 
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ilihesabiwa kuwa 2,083,588.
<ref>[http://www.wavuti.com/uploads/3/0/7/6/3076464/census20general20report20-202920march202013_combined_final20for20printing1.pdf Sensa ya 2012, Mkoa wa Dodoma]</ref>
 
Mnamo Machi [[2012]] ilianzishwa wilaya mpya ya [[Chemba]].
 
==Mawasiliano==
Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia [[mji wa Dodoma]] kwenda [[Morogoro]] - [[Daressalaam]], barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - [[Rwanda]] - [[Kongo]]. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini ([[Arusha]] - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya [[Reli ya Kati]] kutoka Daressalaam kwenda [[Kigoma]] yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.
 
==Hali ya hewa na kilimo==
Kwa jumla Dodoma haina mvua nyingi isipokuwa sehemu za wilaya za Mpwapwa na Kondoa. Hivyo hasa mazao yasiyotegemea sana mvua hulimwa kama vile [[mtama]], [[wimbi]], [[muhogo]]; kilimo cha [[mahindi]] hupatikana mara kwa mara na matatizo ya kukosa mvua. Mazao ya sokoni ni [[karanga]] [[alizeti]] na simsim. Dodoma ni pia mwanzo wa ustawishaji wa mizabibu na uzalishaji wa [[divai]] katika Tanzania.
 
Kutokana na hali ya hewa mifugo ni mingi (ng'ombe 1,600,000, mbuzi 954,000, kondoo 274,000, nguruwe 23,000, kuku takriban 1,400,000). Idadi ya mifugo imeongeza tatizo la [[mmomonyoko wa ardhi]] katika sehemu za Mkoa wa Dodoma.
 
==Wakazi na utamaduni==
Idadi kubwa ya wakazi asilia ni [[Wagogo]]. Kondoa kuna Wangulu na pia [[Wasandawe]] wanaotumia lugha ya aina ya [[Khoikhoi]]. Wanasemekana ya kwamba babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko [[Zimbabwe]] au [[Afrika Kusini]]. [[Kongwa]] kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na [[Mpwapwa]] kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru.
 
==Majimbo ya bunge==
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
* Bahi : mbunge ni [[Omar Ahmed Badwel]] ([[CCM]])
* Chemba : mbunge ni [[Juma Nkamia]] ([[CCM]])
* Chilonwa : mbunge ni [[Joel Mwaka]] ([[CCM]])
* Dodoma Mjini : mbunge ni [[Antony Peter Mavunde]] ([[CCM]])
* Kibakwe : mbunge ni [[George Simbachawene]] ([[CCM]])
* Kondoa Mjini : mbunge ni [[Sanda Edwin]] ([[CCM]])
* Kondoa Vijijini : mbunge ni Dk. [[Ashatu Kijaji]] ([[CCM]])
* Kongwa : mbunge ni [[Job Ndugai]] ([[CCM]])
* Mpwapwa : mbunge ni [[George Malima Lubeleje]] ([[CCM]])
* Mtera : mbunge ni [[Livingstone Lusinde]] ([[CCM]])
 
 
{{Mikoa ya Tanzania}}
 
[[Jamii:Mikoa ya Tanzania|D]]