Tanganyika (ziwa) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
nyongeza kuhusu uwiano wa maji
Mstari 28:
 
==Jina==
Jina la ziwa limepokewa na [[Wazungu]] [[wapelelezi]] wa kwanza kutoka kwa wenyeji wa [[Ujiji]]. [[Henry Morton Stanley]] aliyetembelea ziwa mnamo mwaka 1876 aliandika ya kwamba [[watu]] wa [[Ujiji]] hawakuwa na uhakika kuhusu maana ya jina, ila tu ilimaanisha ziwa kubwa<ref>Habari zifuatazo kutoka HM Stanley, [https://archive.org/stream/throughdarkconti1878stan2#page/n31/mode/2up Through the Dark Continent Vol 2, p 16] </ref>. Maana waliita maziwa madogo "Kitanga", na waliita pia "ziwa la Usukuma" yaani Viktoria Nyanza kwa jina hili "Tanganika". Wajiji walimwambia Stanley ya kwamba labda neno "nika" ilitoka kwa aina ya [[samaki]] walioitwa vile. Baadaye StanleaStanley alikumbuka neno "nika" katika [[lugha]] nyingine za Kiafrika kwa maana ya "tambarare, eneo kubwa bapa" akahisi ya kwamba waliita ziwa kama "tambarare kubwa iliyotanda" <ref>Tanganika, 'the great lake spreading out like a plain', or 'plain-like lake'</ref> .
 
Stanley alishika pia majina ya ziwa kwa [[Kabila|makabila]] mengine- watu wa [[Marungu]] walisema "Kimana", wale wa [[Urungu]] "Iemba" na [[Wakawendi]] "Nsaga" kwa maana "ziwa lenye dhoruba". Alichoshika na watu wa Urungu, yaani "Iemba", inalingana na taarifa ya [[David Livingstone]] aliyekuta jina "Liemba" kuwa jina la sehemu ya [[kusini]] ya ziwa na jina hili linaendelea kutumiwa kwa [[meli]] ya [[MV Liemba]] inayosafirisha watu na [[bidhaa]] ziwani tangu mwaka [[1914]].
 
== Jiografia ==
Maji ya Ziwa Tanganyika yanajaza [[ufa]] kubwa kwenye [[ganda la dunia]] ambalo ni sehemu ya [[bonde la ufa la Afrika ya Mashariki]]. Ni ziwa lenye kina kikubwa katika Afrika.

=== Vipimo ===
Kina cha [[wastani]] ni [[Mita|m]] 570, ni kubwa zaidi katika sehemu ya [[kaskazini]] ambako vilindi vyake hufikia kina cha mita 1470. Kutokana na kina kikubwa kinashika kiwango kikubwa cha maji matamu kati ya maziwa yote ya Afrika (18,900 [[Mita ya ujazo|km³]]) na [[asilimia]] 16 ya maji matamu yote duniani.
 
[[Halijoto]] ya maji usoni mwa ziwa ni [[sentigredi]] 25 na [[uchungu]] wake ni [[pH]] 8.4 hivi.
Line 41 ⟶ 44:
Kina kikubwa cha ziwa kimesababisha kuwepo kwa safu za maji zisizochanganya maana maji ya chini hayakorogwi kwa [[upepo]] au mikondo na maji ya juu, hivyo maji ya chini hayapokei [[oksijeni]] na kuwa na [[uhai]] kidogo. [[Samaki]] na [[viumbehai]] wengi hawawezi kuishi katika maji bila oksijeni.
 
=== Beseni ===
Ziwa linapokea maji yake kutoka [[mito]] ya [[mazingira]] inayoishia humo. [[Beseni]] yake huwa na eneo la km<sup>2</sup> 231,000 (sq mi 89,000). Mito miwili mikubwa na mito mingi midogo inaishia ziwani. [[Mto Lukuga]] hutoka ziwani na kupeleka maji yake kwenda [[beseni ya Kongo]].
 
Mito miwili mikubwa na mito mingi midogo inaishia ziwani. [[Mto Lukuga]] hutoka ziwani na kupeleka maji yake kwenda [[beseni ya Kongo]].
 
Mto mkubwa zaidi unaoingia ni [[Ruzizi (mto)|Ruzizi]] unaofika upande wa kaskazini kutoka [[Ziwa Kivu]]. [[Malagarasi (mto)|Malagarasi]] ambao ni mto mrefu wa pili nchini Tanzania inaingia upande wa mashariki.
 
=== Kubadilika kwa kiasi cha maji ===
Kutokana na mahali pake katika [[tropiki]] kwenye [[jua]] kali, Ziwa Tanganyika linapotewa na maji mengi kwa njia ya [[uvukizaji]]. Kwa hiyo kiasi cha maji ndani yake inategemeana na kiasi cha maji yanayoingia. Kwa sasa [[chanzo]] kikubwa ni maji ya [[Ziwa Kivu]]. Imegunduliwa ya kwamba uwiano wa ziwa ulibadilika sana katika [[historia]]. <ref>[https://books.google.de/books?id=C_ABrmnsKY4C&printsec=frontcover&dq=L%C3%A9v%C3%AAqu,+Christian&hl=de&sa=X&ved=0ahUKEwibw9GtyJTQAhVCJsAKHYBLDWwQuwUINTAC#v=onepage&q=L%C3%A9v%C3%AAqu%2C%20Christian&f=false<nowiki> tazama Christian Lévêque, Biodiversity Dynamics and Conservation: The Freshwater Fish of Tropical Africa], Cambridge University Press 1997, uk. 109 ff</nowiki>von C.</ref>
 
Line 51 ⟶ 58:
Hali ya sasa imepatikana tangu miaka 12,000. Wakati ule [[volkeno za Virunga]] vililipuka na kuziba mto uliowahi kubeba maji ya Ziwa Kivu kuelekea [[mto Naili]] na baada ya kufikia uwiano wa leo maji ya Kivu yalianza kutoka upande wa Tanganyika kupitia njia ya Ruzizi.
 
Mabadiliko ya uwiano wa maji kwenye ziwa zilitazamiwa pia katika historia ya miaka 200 iliyopita kwa kulinganisha kumbukumbu ya wakazi na taarifa za wapelelezi wazungu walioandika taarifa juu ya safari zao. Baada ya mwaka 1800 maji yalikuwa chini sana, kabla ya 1900 yalikuwa juu sana, tangu 1900 yalishuka tena. Katika miaka ya 1960 ziwa lilijaa tena likabaki hivi hadi sasa. Mabadiliko haya yanalingana na mabadiliko katika kiasi cha mvua inayopokelewa katika beseni ya ziwa. <ref>[http://link.springer.com/article/10.1023/A:1005424619718<nowiki> Historical and Modern Fluctuations of Lakes Tanganyika and Rukwa and Their Relationship to Rainfall Variability], Sharon E. Nicholson in: Climatic Change (1999) 41 (sumarry on springer.com, iliangaliwa Novemba 2016)</nowiki></ref>
 
=== Miji na nchi jirani ===
[[Miji]] mikubwa ziwani ni [[bandari]] za [[Kigoma]] kwa upande wa Tanzania na [[Kalemie]] kwa upande wa Kongo. Kila bandari ni pamoja na mwanzo wa [[njia ya reli]]. Mji mkubwa kabisa ni [[Bujumbura]], [[mji mkuu]] wa [[Burundi]].
 
Eneo lote la ziwa limegawiwa baina ya nchi jirani yaani [[Tanzania]], [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]], [[Burundi]] na [[Zambia]]. Sehemu kubwa iko chini ya Tanzania (46[[%]]) and J.D. Kongo (40%).
 
==== Visiwa ====
Kuna [[visiwa]] mbalimbali ndani ya ziwa Tanganyika. Vikubwa zaidi ni pamoja na
* Visiwa vya [[Kavala]], [[Mamba-Kayenda]], [[Milima (kisiwa)|Milima]] na [[Kibishie]] katika sehemu ya J.D. Kongo