Magindu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
+kiungo
Mstari 22:
Magindu imepakana na [[Wilaya ya Morogoro vijijini]] kwa upande wa kusini na magharibi, kata ya [[kwala]] kwa upande wa mashariki na Mji wa [[Chalinze]] kwa upande wa kaskazini. Kijiji cha Magindu kilitokana na neno la [[Kikwele]] "ng'indu" lenye maana ya kima kwa Kiswahili waliopatikana kipindi cha ujenzi wa [[reli ya kati]] toka Dar kwenda Kigoma iliyopitia kijiji hapo.
 
Wakazi wa kijiji na kata ya Magindu ni mchanganyiko wa [[Wakwele]] na [[Wamaasai]] hususani vijiji vya Gumba, Gwata na Magindu pia wakutu wanaopatikana kijiji cha Lukenge. Kijiji cha Magindu ni moja ya vijiji vichache vilivyojariwa rasilimali watu, misitu na ardhi ya rutuba. Wanakijiji wa Magindu kama ilivyo vijiji vingine Tanzania wana mila na desturi za kabila lao la Wakwele na hucheza ngoma za Jando[[jando]] kwa wavulana na [[uny'ago]] kwa wasichana ambazo mara nyingi hufanyika kipindi cha mavuno au mlao kama inavyojulikana huko.
 
Magindu ni kijiji ambacho pia kimejaliwa kupata huduma muhimu za kijamii kama shule ya msingi na sekondari, kituo cha afya na barabara yenye kiwango cha kokoto inayounganisha Magindu na Chalinze ya [[wilaya ya Bagamoyo]] ila bado kuna tatizo la umeme ambao serikali imeanza mipango ya kupeleka umeme huko. Vitongoji vya Magindu ni Mizuguni ambacho ni kijiji kipya, Magindu mjini, Lukarasi, Mnyonge na Kuyu.