BBC : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Idhaa ya Kiswahili
Mstari 13:
}}
[[Picha:BBC Broadcasting House Portland Place.jpg|thumb|BBC Broadcasting House, [[London]]]]
The '''British Broadcasting Corporation''' (BBC) ni shirika la utangazaji la [[Uingereza]]. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1922 kwa jina la [[British Broadcasting Company Ltd]] kama kampuni binafsi. Baadaye mwaka 1927 lilibadilishwa hadhi yake na kuwa shirika la umma. BBC ndio shirika kubwa la habari kuliko yote duniani likiwa linatoa habari na taarifa mbalimbali kwa njia ya redio, luninga, na Intaneti. Tangu 1957 imerusha habari kwa Kiswahili.
 
==Lengo na utawala==
Kwa mujibu wa BBC, lengo lake ni kutoa habari, kuelimisha, na kuburudisha. Kauli mbiu yake ni "''Nation Shall Speak Peace Unto Nation''."
 
Shirika hili linaongozwa na [[Bodi ya Magavana]] wanaochaguliwa na [[Malkia]] au [[Mfalme]] wa Uingereza kwa ushauri toka kwa mawaziri wa serikali ya Uingereza. Hata hivyo, BBC inasema katika katiba yake kuwa inafanya kazi zake bila shinikizo toka kwa wanasiasa au wafanyabiashara na kuwa linawajibika kwa wasikilizaji na watazamaji wake tu.
 
==Idhaa ya Kiswahili==
Matangazo kwa lugha ya Kiswahili yalianza mwaka 1957. Tarehe 27 Juni 1957 sauti ya Kiswahili ilisikika mara ya kwanza; msemaji alikuwa [[Oscar Kambona]] aliyekuwa wakati ule mwanafunzi wa chuo kikuu huko London na baadaye [[waziri wa mambo ya nje]] wa kwanza baada ya uhuru wa Tanzania.<ref>[http://www.thecitizen.co.tz/oped/MUGERA--BBC-Swahili-s-East-Africa-homecoming/1840568-2415072-hc99tez/index.html MUGERA: BBC Swahili’s East Africa homecoming], The Citizen Monday, August 11, 2014, kmeangaliwa 2016-12-03</ref>
 
Idhaa ya Kiswahili ya BBC imepanuka huduma zake hadi televisheni na intaneti. Tangu 2014 imehamisha ofisi na programu zake zote kuja Afrika ya Mashariki, ikirekodi Dar es Salaam na Nairobi.
 
== Viungo vya nje ==
* [http://www.bbc.co.uk/swahili/ Tovuti ya Idhaa ya Kiswahili BBC]
 
<references/>
 
 
{{commonscat}}